Kwa masikitiko nauona mwisho wa chama changu CCM

Kwa masikitiko nauona mwisho wa chama changu CCM

Ila naye alikuwa mnafki kutuharibia "katiba mpya" na uchaguzi wa 2015. Hivyo siuoni uzalendo wake

Hajaharibu katiba mpya

Mchakato wa katiba ambao ulikuweko kwa mujibu wa sheria ulikuwa umebakiza zoezi la kura ya maoni tu ili tupate katiba mpya.

Sasa kura ya maoni isingeweza kupigwa mwaka 2015 wakati tulikuwa na zoezi la uchaguzi mkuu, hayo mazoezi yote mawili yalihitaji maandalizi, muda na fedha na NEC wakasema wasingeweza kuyasimamia yote kwa pamoja.

Tulitegemea Rais Magufuli alipoingia madarakani ndani ya miaka 2 angeweza kumalizia kipengele cha kura ya maoni juu ya rasimu ya Chenge iliyokwishapitishwa kwenye bunge la katiba ili tupate katiba mpya!

By all standards rasimu ya Chenge ilikuwa ni nafuu kuliko katiba ya sasa
 
Kwa maoni yako tukubali katiba yetu ya sasa ni mbovu kupindukia. Kama jambo la muhimu kwa taifa , linaachwe kwenye utashi wa Rais bila maelekezo !!. Basi ataendelea kusema si kipaumbele chake.

Katiba yetu imemrundikia Rais mamlaka na majukumu yaliotakiwa kufanywa na taasisi . Only in Africa
 
Hizi ndio akili zetu wengi wana CCM.
[emoji23] [emoji23] Kweli kabisa mkuu, yaani wameaminishwa kwamba watatawala milele, they don't want to look outside the box [emoji1003]...
 
Tatizo kubwa la ccm ni kumruhusu Mwenyekiti wenu kuwa bz na media kwa miaka 4 uku mkiwaziba wapinzani mikopo. Leo hii tunakwenda kuanza kampeni, Mgombea wenu ladha yake machoni na masikioni kwa wapigakura imezoeleka, wakati Tundu Lissu amekuja kama chakula au kinywani kipya chenye kuvutia na kupendeza machoni pa wengi, hapo kila mtu atataka kumwona na kumsikiliza.

Sishangai ccm kuwakusanya wanamuziki zaidi ya 40 na kuwazungusha ili wawavutie watu waje kwenye mikutano yao. Hiyo ni dalili ya chama kilichoishiwa na kufilisika kifikra.

Mchimba kaburi huingia mwenyewe, hii hali ya sasa ya kisiasa mliitengeneza wenyewe na sasa mnapaswa muikabili
Mkuu popote ulipo pata kinywaji and bites of your choice [emoji120][emoji120][emoji120][emoji106][emoji106][emoji106] this is exactly what I have been telling people....
 
Kweli ni lazima mtu awe mjinga kuwa mwanachama wa Chama cha CCM au akijiunga na Chama akiwa na akili zake, ubongo utaoshwa mpaka awe mjinga sawa na wenzake. Angalia huyu ameorodhesha madudu yote yanayofanyiwa Vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla anasikitika sana eti lichama libovu kama hilo linakwenda kufa. Si life tu kwani Watanzania wote ni wanachama wa chama vha siasa au kama ana mkataba nalo si avunje tu au kama damu yake ni kijani, si aende hospitali wambadilidhie apate yenye akili? Hakuna Chama chenye hati miliki ya kuongoza kinavyotaka bali kiongoze kwa matakwa ya wananchi waliokiweka madarakani vinginevyo kitupiliwe mbali hakifai.
 
Chama kama chama hakina shida, shida siku zote ni watu
 
[emoji23] [emoji23] Kweli kabisa mkuu, yaani wameaminishwa kwamba watatawala milele, they don't want to look outside the box [emoji1003]...
Lazima tuangalie mifano ya vyama kama vyetu vinavyoitwa vya ukombozi vinazidi kutoka . Siku zimebadilika, sera ni maendeleo ya watu na uchumi.
 
Jambo hili linaloumiza nililiona tangu kuanza kukataliwa kwa mikutano ya siasa na kuletwa kwa sheria mbalimbali kama za takwimu, habari n.k ambazo kiuhalisia lengo ilikuwa kudhibiti ukosoaji na Upinzani na kuongeza kuungwa mkono kwa chama na serikali kwa sababu watu watakuwa wanasikia mambo mazuri yaliyofanyika peke na kujenga mawazo chanya kwa serikali.

Hii ilikuwa kama kucheza kamari kwa sababu inaweza kulipa kisiasa au ikarudi kukuumiza. Kichama mwanzoni haya yalikuwa maamuzi mazuri kwani lile vuguvugu la 2015 na watu wangeachwa waongee muda wowote basi ingehatarisha kupungua kuungwa mkono na wananchi kwa chama na Serikali kwa ujumla.

Lakini sheria hizo na katazo halijakisaidia kuungwa mkono zaidi Chama na serikali kwa ujumla bali limeghairisha tu kwa muda, Chama kimebweteka kikitegemea dola kunyamazisha mawazo tofauti na wakosoaji. Kimeshindwa kujitathmini sera zake na uungwaji wake mkono na wananchi. Matokeo yake kimekuwa 'surprised' muitikio wa watu kwa upinzani kipindi hiki.

Hatujui tuseme nini, maana tulishasema kwa miaka bila kupewa changamoto. Kama tuliwaambia yale yale lakini sasa hivi tunaona kumbe hawajelewa je sasa hivi tutaambia nini cha tofauti? Mtumishi hajapanda daraja tunamwambia tunajenga bwawa, mpinzani anamwambia ni haki yako umeikosa kwa miaka minne . Mwananchi kijijini tutamtajia kuwa mafaniko tumenunua shirika la ndege, mpinzani atamwambia mji hujaletewa miaka miaka minne. Hakuna uchawi hapo.

Upinzani wana kazi rahisi sana,wanazungumza na kufanya yale ambayo watu walizuiwa kwa miaka minne , wananchi wanaona faraja wamepata wa kuyazungunza na kuamsha ari zao. Watu hawakutegemea kuwa wapinzani wangevuta watu na husia zao kiasi hiki. kamari ya kuzuia mikutano na kutofanya siasa ime 'backfire' inatuumiza sisi.

Tungewaacha waongee miaka yote watu wangeona hawana jipya wangezoea tu kama miaka yotr. Ni wazi wananchi wana mengi sana wameweka moyoni, wana matatizo wana manung'uniko mengi, si waalimu, si wanafunzi, si wafanyabiashara wala si wakulima. Sote tunajua hali halisi. Watu wanavinyongo moyoni ila pakusema hakuna.

Lakini lingine, ikatokea chama kikaendelea kushika dola baada ya uchaguzi 2020. Na aliyepo akaondoka 2025, uwezako mkubwa ni hizi sheria makatazo na hatua za kuzuia mawazo mabadala mengi yataondolewa, hapo sasa ndipo itakapokuwa rasmi chama kimemalizika.

Hebu fikiria miaka hii minne walimu, wafanyabiashara, wanafunzi vyuo vikuu wakulima na watumishi kwa ujumla wangekuwa huru kutoa madukuduku yao, fikiria vyombo vya habari vinatoa fursa sawa kwa wapinzani kusikika, fikiria press comference hazizuiwi n.k nadhani tunapata picha halisi kuwa chama kipo katika haoi mbaya ya uungwaji mkono kisiasa. Tukitoboa 2020 basi 2025 napata mashaka sana.

Lissu tumtengeneza wenyewe, Lissu alishamkosoa sana JK kama Rais mwenyekiti wa Chama na kama mtu binafasi lakini tuliomuoma kama tu mpinzani anayeongea sana kama wengine tu , ikulu aliitwa na chai anakaribishwa. Ila sasa hivi Lissu anaonekana shujaa mbele ya wananchi, kwanza ame survive assasinationa attempt na mbili anazungumza yale madukuku yaliyojaa moyoni. Lissu wa sasa sio yule ana nguvu kubwa ya ushawishi, ni kwa sababu tu anazungumza yanayowagusa wananchi. Lissu anatisha.

Busara inahitajika kunusuru taifa, tusilazimeshe mambo, Taifa letu litabaki vyama vitakuja na kuondoka. Lazima tukubali ukweli kuwa iko siku chama kitatoka madarakani, sisi wa kwanza kwa vyama vya ukombozi kutolewa kwenye dola. Na tujiandae kisailolojia kuwa siku za kuwa chama dola zimekaribia mwisho, tukijisahaulisha haya ndio tunahamaki badala ya kukabiliana nao kwa hoja tunafanya ya tofauti.

Chondechonde yaliyotokea Hai ni aibu na fedheha kubwa yasijirudie kwa sababu mwisho wake sio mzuri, tujiulize kwa nini anavutia watu wengi, kwa nini wanamsapoti, kwa nni wanamsikiliza. tufanye propanga na mbinu zingine ila sio ya Hai. Uzalendo ni kusimama na Taifa sio na Chama au Mtu, tusiwe tayari kunyamazisha wapinzani kwa njia ambazo zitagharimu Taifa wala usiwe tayari kuona Taifa linaangamia kwa sababu tu kulinda chama au mtu.

Sidhani kama kuna tafsiri mpya ya Uzalendo.

Tanzania yetu ni moja.
Wacha wayaone wenyewe. ASANTE MUNGU KUTULETEA RAIS WA UKWELI TAL
 
Back
Top Bottom