Pre GE2025 Kwa maslahi mapana ya nchi ya Tanzania, Wabunge hawa hawatakiwi kukosa kwenye bunge la 2025-2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bando la wiki

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2023
Posts
911
Reaction score
3,017
Huu ni utabiri juu ya nini kitatokea 2025 hadi 2030, itakuwa ni wakati wa kuwakomoa watanganyika. Nchi itapigwa mnada bila hofu yoyote kwa sababu watanganyika hao hao viongozi ndio wanasapoti uuzaji huo uendelee.

Wananchi wa Ngorongoro wataondolewa ngorongoro wapende wasipende. Rasilimali muhimu za nchi kama misitu na madini hifadhini yatachibwa na wageni bila faida ya muda mrefu kwa vizazi vya kitanzania.

Hivyo kwa maslahi mapana ya taifa la Tanganyika wabunge wengi wa upinzani wanaitajika sana kwenye bunge la 2025 -2030.
Kwa mfano bunge siku za hivi karibuni limekuwa likiendelea pasipo wananchi kutokujua kwamba linaendelea, hivyo kupitia udhaifu huo bunge limekuwa likipitisha mambo mengi ya hovyo ambayo ni mzigo kwa wananchi wengi wa taifa hili. Mfano mzuri sasa hivi LUKU mwananchi wa kawaida analipia Kodi ya Thamani (VAT) wakati huo huo tunalipa matozo mengine ya ajabu kwenye LUKU hiyo hiyo (debt collection kutoka 1000 hadi 1500 ambayo TRA walikanusha kwamba hawahusiki kuikusanya). Hivyo tungekuwa na bunge la wazelendo mambo ya hovyo kama hayo ma double taxation yasingepitishwa na bunge letu tukufu.

Watu muhimu ambao wanapaswa wananchi tuwapeleke bungeni ni;
  • Joseph Mbilinyi (Sugu)
  • John Heche
  • John Mnyika
  • Godbless Lema
  • Boniface Jacob
  • Tundu Lissu: huyu kiongozi hatakiwi kukosa kabisa bungeni. Kama chama kingeruhusu huyu kiongozi angegombea nafasi ya urais na ubunge kwa pamoja. Tundu Lissu ndie kiongozi pekee kwa upinzani anaweza kupambana na kiongozi yeyote wa CCM ngazi ya urais na yeye akaibuka mshindi. Lakini endapo atahujumiwa kwenye nafasi ya urais tusimkose kwenye bunge la 2025- 2030 atatusaidia sana kuzuia sheria mbovu na Madudu mengi.
Wengine wa kuingia bungeni ni pamoja na;
  • Peter Madeleka
  • Peter Kibatala
  • Boniface Mwambukusi
  • Luhaga Mpina.
  • John Pambalu
  • Twaha Mwaipaya
  • Ado shaibu
  • Aida Khenani
  • Catherine Ruge
Pamoja na mimi na wewe kama unahisi unao uzalendo wa kulipambania taifa la Tanzania na wananchi wake ili waweze kuumiliki uchumi wao.
 
Huyu Wenje si ndio dalali wa kumpeleka mtoto wa Samia aitwae Abdul kwenda kuwahonga wakina Lissu fedha ili wasimuumbue mama yake na madudu anayo fanya na wajomba zake waarabu kuhujumu nchi!!
Wenje haaminiki ni mamluki.
 
Kwenye orodha yako sijaona waislam wala wanawake. Vipi kwa mtazamo wako hawafai?
 
Ninaunga Mkono Hoja kwa AsilimiašŸ’Æ%
 
.......wengine ni:
* Aida Kenan
* Kina Ester wote..i.e Bulaya na Matiko
* Halima Mdee
* Hussen Bashe
* Condester Sichwale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…