Habari zenu wana jf kwanza kabisa napenda kuishukuru serikali yetu kwa kutuletea matokeo mapya, kuna wengi wamefurahishwa kutokana na matokeo hayo ikiwemo wanafunzi, wazazi pamoja na walimu ila mi kwa upande wangu sijafurahi wala sijachukia kwasababu matokeo ya mwanzo nilikua na 4 ya 27 na sasa nina 3 ya 24 civ-d hist-f geo-d kisw-c eng-c phy-d chem-c bio-c math-d lakini sina hata comb moja iliyobalance. Hivyo napenda msaada wenu wana jf inawezekana mimi nikaenda advance kusoma pcb? Na inawezekana nikachaguliwa kusoma shule ya serikali maana nimetoka shule ya kata.