Kwa mazingira haya bado tunaweza kuiita Sensa ya Watu na Makazi?

Kwa mazingira haya bado tunaweza kuiita Sensa ya Watu na Makazi?

Abdideol

Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
13
Reaction score
6
Hivi sensa itamuhesabu vipi yule Mtu anayelala Darajani Salenda au kwenye Mabaraza pale Manzese? 🤔

Ikiwa tunasema ni sensa ya watu na makazi?

Na itakuaje kuhusu bajeti ya mtu huyu baada ya yeye kutokuhesabiwa kwa kuwa hana makazi maalumu na darajani pale au sokoni ambapo anapatikana wakati wa usiku hapakuwekwa postikodi kwa maana ya makazi maalumu?

Vipi ikiwa siku za usoni mtu huyu atapata watoto inakuaje bajeti ya mtu huyu?
 
Hao wanaolala vibarazani wana dodoso lao!
Acha kukurupuka na hili andiko lako!
Wataalamu walishalijua hilo kabla!
 
Kwenye sensa pia kuna makadirio, huyo atawekwa kwenye makadirio, kama sijakosea idadi ya watu ikipatikana kuna namba kadhaa wanazikadiria kuziba ambao hawakuhesabiwa.
Lakini nafikiria wakiwa zaidi ya Makadirio waliyoyafanya wao.??
 
Acha uongo nipo kwenye kamati ya sensa mzee hakuna kitu cha dodoso lao na hakuna sensa itakayo hesabiwa Usiku hao wanao lala mabarabarani huwa wanapatikana usiku tuu na si mchana so jaribu kuwa na majibu na kauli nzuri kwa mtu anae uliza swali
 
so unataka na wanaolala mitaroni nao tuseme makazi
 
Acha uongo nipo kwenye kamati ya sensa mzee hakuna kitu cha dodoso lao na hakuna sensa itakayo hesabiwa Usiku hao wanao lala mabarabarani huwa wanapatikana usiku tuu na si mchana so jaribu kuwa na majibu na kauli nzuri kwa mtu anae uliza swali
[emoji23]

Upo kwenye kamati ya sensa ngazi gani?
 
Acha uongo nipo kwenye kamati ya sensa mzee hakuna kitu cha dodoso lao na hakuna sensa itakayo hesabiwa Usiku hao wanao lala mabarabarani huwa wanapatikana usiku tuu na si mchana so jaribu kuwa na majibu na kauli nzuri kwa mtu anae uliza swali
Hakika Mkuu
 
Hii sio sensa ya kwanza hivyo wataalam wanajua wakifanyacho
 
Watu wasio na makazi maalumu watahesabiwa Usiku tu wako na Dodoso lao inshort Serikali imejipanga
 
Kweli huhesabiwa usiku wanapo lala, iwe kibarazani, stand za mabasi, darajani, mitaroni, n.k hao wote watahesabiwa kama kundi maalumu, hata wale dada zetu wa usiku nao watahesabiwa kama hawa 😅

anayebisha hapo juu awe na sababu za kujitosheleza au akaulize watu wa NBS wampe muongozo wa hili, mijitu mibishi. No research no right to speak mazafanta kabisa.
 
Back
Top Bottom