Kwa mechi hizi.. Hakuna timu ya kumzuia Simba S.C ....

Kwa mechi hizi.. Hakuna timu ya kumzuia Simba S.C ....

Yaani nyie mashabiki wa simba mna akili ndogo sana, mnaamini kufungwa kwenu ni refa kawafungisha sio sehemu ya mpira, ingekua timu yenye uwezo haifungwi basi hata barca isingefungwa, jifunzeni basi kupitia hata kwa jirani
 
Hatimae yule Mnyama mkali, mwenye nguvu na makucha makali pengine kuliko wanyama wote mwituni.. Simba kamaliza nusu ya raundi ya kwanza ya VPL kwa kishindo kikuu.

Kamaliza hii duru kwa staili ya pekee kabisa..
1. Akiwa kileleni
2. Akiwa hajapoteza mechi hata moja
3. Akitafuna kila kitoweo kilicho mbele yake
4.Akitandaza soka maridadi kabisa, ambalo limekua gumzo Africa Mashariki na Kati [CECAFA] n.k

Ili kumalizia raundi ya kwanza ya ligi kuu, msimu huu.. Mnyama kabakisha mechi hizi;
15.10.2016: Simba S.C Vs KAGERA SUGAR
20.10.2016: Simba S.C Vs MBAO FC
23.10.2016: Simba S.C Vs TOTO AFRICAN
29.10.2016: MWADUI FC Vs Simba S.C
02.11.2016: STAND UNITED Vs Simba S.C
06.11.2016: AFRICAN LYON Vs Simba S.C

NOTE:TANZANIA PRISONS Vs Simba S.C.. Itapangiwa Siku.

Ukiangalia hizo mechi 8 zilizobaki kwa umakini mkubwa.. Utagundua hakuna timu yenye uthubutu wa kumzuia Mnyama, kumaliza raundi ya kwanza ya ligi msimu huu akiwa kileleni.

SIMBA SPORTS CLUB.. NGUVU MOJA.


Watu hupenda kusahau historia...wakati kama huu msimu uliopita Simba ilikuwa position gani na mwisho wa msimu Simba ilikuwa position ipi??? Fikiria sana...Mechi nane watu mnaanza kuzungumza???? Duh
 
Simba damu naipenda sana timu yangu hii. go go go go mnyama
 
Simba hii ni kanyaga twende.
 
Kagera sugar na stand united je?
 
Nyie simba ongeeni sana ila jueni kambarage hamtoki.Ushindi wenu kambarage ni dro😵va
 
Kichuya na Ajibu ni hazina ya taifa inabidi tuilinde ipasavyo kama tanzanite tu
 
Mahaba Niue.. Kuna mzungu mmoja wa simba mwaka jana alisema tukutane mwezi May kama Simba hatakua Bingwa... Sasa naona picha linajirudia,. Na sisi tumewazoea.. Twenzetu.
 
Mkuu.. wewe mwenye ufahamu wa hali ya juu sana kuhusu mpira ulivyo, unaonaje ukatutoa tongo tongo sisi tunaoshabikia kwa kufuata mkumbo?
Wahenga wana msemo wao.. "ulichopewa bure.. toa bure".
ww unadhan kila mjinga huwa anaelishwa?,
 
Back
Top Bottom