Kwa mechi ya jana misri vs Tanzania tujiandae na saikolojia

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,654
Nimeangalia mechi ya jana usiku nikajuta kupoteza usingizi wangu

Jana tulikuwa na mchezaji moja tu ambaye ni manula angalau na beki imejitahidi kwa kiwango kidogo unaweza sema manula aliperform kwa 8/10 beki 4/10
Ila kuanzia katikati kwenda mbele ni 1/10

Yani wachezaji wetu walikuwa wanabutua halafu kiungo tumewekewa wapuuzi eti Himid Mao na feisali???
Hivi huyu Kocha anatuona sisi hatujui sana mpira?
Mao lini akawa mchezaji mzuri kuliko mkude pale katikati?
Feisal hajjui kukaba hajui kuichezesha timu ndio anaitwa middle inayoanza kuliko wachezaji wote!!
Timu dkk zote 90 inabutua mpira na Kocha Hana hata plan B

Hili Kocha tahira mlilitolea wapi?

Tukifungwa goli saba kila mechi tustaajabu sioni timu ya kutoa sare hata na Kenya kina samata na kina msuva tunaowategemea kuichachafya ngome ya wapinzani ndio waligeuka wakabaji huku wakiwa wamepooza na viungo kina humid na feisal wanajificha kwenye migongo ya wachezaji wa misri

Amunike wewe ni mpumbavu kabisa

Nilitamani maximo arudi hata kwa mwezi tu
 
Amunike HAFAI na anatupotezea Muda tu.
Baada ya kuona Misri wametutawala kwenye kiungo, kulikuwa na haja gani ya kumuingiza Ulimwengu? Pale ilitakiwa wabaki washambuliaji wawili tu mbele: Samata na Msuva halafu angeimalisha kiungo kwa kuweka wakabaji na watoa pasi za mwisho kama Mudathir na Domayo. Vilevile angalau angemweka Erasto namba 6 ili atulize timu.
Badala yake anachezesha beki wawili wa kushoto kwa mpigo: Tshabalala na Gadiel!! Huu mfumo wa wapi??????
Timu inabutua tu, hakuna structure au pattern inayoeleweka, yaani tunavyocheza hata dunia itatushangaa tuliingiaje Afcon!
TFF TUONDOLEENI HUYO BOYA AMUNIKE BAADA YA AFCON, ANATUHARIBIA TIMU TU.
 
Nina maoni tofauti. Mimi binafsi siridhishwi na style na personality ya Amunike. Lakini hii haininyimi nafasi ya kuona ubora na uzuri wa kitu anachokifanya na timu inavyocheza.

Kwanza timu imecheza kwa mfumo mzuri unaoeleweka. Wamekaba vizuri hasa kuzuia krosi za Wamisri japo walifanikiwa kupiga krosi kadhaa na kupata goli kwa mojawapo ya krosi hizo. Wachezaji wote wamecheza vizuri na wameonyesha ushindani. Timu ina mwelekeo sahihi, lakini kocha akubali kubadilika kidogo, apokee ushauri ili timu ifanye vyema zaidi.

Kwanza, ni kweli huwezi kucheza na timu ya kiwango cha Misri halafu eti ukataka mgawane possession! Hatujafikia kiwango hiki, kwa hiyo approach ya mwalimu ni sahihi. Lakini tatizo ni nafasi anazowapanga wachezaji. Anapocheza John Bocco alipaswa kucheza Simon Msuva.

Msuva ana kasi na maamuzi ya haraka, anahitaji eneo kubwa kwenye mianya ili kuisumbua defence. Anaweza kujaribu kukaba kiasi fulani kwenye winger (tracking), lakini uwepo wake eneo la kulia ni dhahiri timu ya Misri ingerudi nyuma angalau upande ule.

John Bocco, ana kimo, na nguvu. Anaweza kusimama katikati ya mabeki wawili nao wakakosa raha hasa kwa mipira ya juu. Ni mzuri anapotokea katikati na kuivuta timu kulia. Timu ikipangwa hivi ule utulivu wa defence kupanga mashambulizi kama walivyofanya Wamisri usingekuwepo. Kumpanga Bocco kama winga wa kupanda na kushuka, ni matumizi mabaya ya rasilimali watu uwanjani.

Kuhusu defence, Amunike anataka timu ianze kucheza mpira nyuma. Bahati mbaya Aggrey Morris si mzuri katika hili. Mbaya zaidi kiungo wa chini Himid Mao si mzuri pia wa kutawala mpira na kuichezesha timu. Pressing ya Wamisri kwenye kiungo ilikuwa kubwa sana, na bahati mbaya timu yetu haigusi pasi mojamoja ya haraka, na ndio maana mipira ikawa inapotezwa kwa haraka. Hatuwezi pia kuificha mpira isipokuwa Samatta pekee ndio alikuwa akikaa na mpira unakuwa salama kiasi fulani.
Hapa ndio Erastho Nyoni anapohitajika kuwa kiungo wa ulinzi ambaye anakaba, na kuituliza timu. Tungeweza kuupata ubora wa Feisal Toto zaidi ya vile. Viungo wangekuwa wanapiga pasi ndefu pembeni kulia kama Msuva angekuwa anapitia kule.

Amunike ajaribu, machache tu, Bocco katikati, Msuva kulia na Nyoni kiungo, timu italeta kitu fulani kizuri zaidi ya sasa.
 
Sijaangalia mpira niliangalia statics. Umiliki mpira ni zero kabisa.
 
Kiungo pale naona ni yule dogo wa Azam Mudathir nae hakucheza jana
 
Erasto na Mudathir hawa ndio walicheza mechi ya Uganda walipeleka timu mbele lakini jana hakuna hata pass 2
 
Watanzania kwa lawama. .Waarabu hata hao magiant Nigeria, Ghana ,Senegal hawawezi kushindana nao kwenye kumiliki mpira. .wao walichofanya Samatta asitembee na wakafanikiwa. .mambo ya wakina Mkude na Ajibu achaneni nayo. .next match na Zimbabwe tutaona utofauti. .Mara zote tunapata tabu sana kucheza na waarabu. .ila weusi wenzetu hata Senegal bila ya Mane tutawachakaza na Kenya pia..mechi ngumu kwetu wale Algeria
 
Mimi nasema ya kwamba Taifa Stars jana ni kweli walizingua hilo sikatai ila kusema ya kwamba 'Samatta na msuva' ambao ndio washambuliaji wetu wa jana.

Eti kusema ya kwamba walizingua nakataa kwa herufi kubwa "HAPANA" kwasababu kama wewe kweli ulikuwa umeuangalia kweli ule mpila washambuliaji wetu hao walikamatwa na tena ki sawa sawa.

Nimeshuhudia zaidi ya mara 5 watu watatu mpaka wanne wanaoneshwa wanamkaba samatta mtu mmoja. Hii ikimaanisha ya kwamba wanajua uwezo wake upoje na ndio maana wakawa wanajihami sana na kama wakivunda kidogo tu akawatoka basi anafanya shambulio zuri. Hivyo tusiseme ya kwamba eti washambuliaji wetu walivuruga mimi nakataa. Ila tuseme ya kwamba beki ya Egypt ilikuwa vizuri sana.

Lakini pia pongezi kubwa ziende kwa kipa wetu pamoja na mabeki kwani wao ndio waliofanya kazi kubwa sana kuliko midfielder walikuwa wanafanya upuuzi tu uwanjani kwani mipila mingi ilikuwa inapotea kati kati na ndio sababu iliyofanya mabeki wakipata mpila ni bora kuanua ufike mbele huko kwani hiyo ndio sifa ya beki.

Na jana kikosi cha Egypt kilijaa nyota wao wote yani ambao hawajaingia hata watatu hawafiki likiwemo jini lao Sarah
Kwani hata sub wenyewe ndio walifanya nyingi Sita (6) na sisi tukafanya (2) tu.
 
Kwani mechi ilikuwa na limitation ya sub? Kuna aja gani ya kubaki na faisali salumu wakati uko mbele Msuva na samatta awapati mipira? Kwanini ajaingizwa mudathil Yahaya na Domayo ili wawalishe mipira samatta na msuva kule mbele? Shaba kessy alikuwa kachoka kitambo Zimbwe junior alitakiwa kuingia mapema. Je kwanini Morris akutoka mapema ili Nyoni afanye yake pale nyuma akiwa na Yondani? Pale atuna kocha ila kuna tourist kaja kuyasoma mazingira ya Tanzania. Yani dakika tisini zote golikipa wa misri kadaka mipira miwili tu? Hapana atupo sirious na mpira.
 
Kama Stars imefungwa 1-0 pongezi kubwaaaaa kwa amunike . Ametufikisha mbali sana. Misri ndiyo bingwa mtarajiwa wa mashindano haya , kumbuka mwaka jana walikuwa kombe la dunia.zamani tulikuwa tukifungwa 5-0 na misri. Kufungwa moja tu tumefanya kazi ya ziada kama vile tumeshinda. Vile vile vijana walikuwa hawajapiga kambi muda mrefu ili kuelewana . Amunike ongezewe mkataba wa miaka 5. Kubadilish wachezaji na position ilikuwa nia ya Kocha ili aone kama kuna badiliko.
Kenya tunawafunga, Senegal tunawafunga au droo . Algeria watatupa shida kidogo . Aina ya uchezaji wa Algeria na misri ni Sawa Mpira wa kazi .
Yote kwa yote sijaona Dalali mbaya bado.
Tatizo la Tanzania kila mtu ni mtaalamu wa mpira.
Kuna mtu yoyote hapa jukwaa la Michezo au Tanzania Anajua Mpira kuliko amunike?
Amunike amechukua kombe la afrika Enzo hizo kuna kina roger Mila , yeboah, abedi pele , hossam Hassan , kalusha nk
Amecheza kombe la dunia na maradona Nigeria ikaisumbua Argentina ya maradona sio Argentina ya messi na di maria
 
Kocha atakuwa amemficha Mudathir kwa kazi maalum
 
unamfaham Pepe wa lille wewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…