Kwa mechi ya jana misri vs Tanzania tujiandae na saikolojia

Salute mkuu.
Haya ndio maoni ya kiunamichezo.
 
Mripa haupo bila mashabiki.

Nianze na wewe mtoa mada umecheza 0/10 ya wajibu wako.

Sababu:
1. Natanguliza disclamer kwani sina CV yako, lakini kwanza ulipaswa kulinganisha vitu vinavyolingana, (Misri na Tz) na pia (wewe na Amunike!!!?) eti wewe unamkosoa Kocha kwa uelewa wa mpira upi unaoujua. Lakini si wewe tu bali wa Tz wengi wanajua mpira wa maneno. Tz kimpira tupo mbali (chini) sana na mpira wa leo ni wa kisayansi na mpira ni pesa na uzoefu. Sasa linganisha vyote hivyo vya misri na sisi wapi na wapi?
2. Ulipaswa kazi yako kubwa iwe kuwatia moyo vijana wetu na umeshindwa na kukosa fadhila. Tilia maanani kuwa kwa timu zetu hizi changa mpira kwa mchezaji ni kujitolea na kuna uwezekano akavunjika mguu na biashara ikawa imeishia hap hapo lakini bado wewe unawalaumu kama vile umewalipa.
3. Tusisahau malengo yetu mpaka sasa ni kuweza kufika finali hizi za African cup of Nations na Amunike kafanikiwa hata kama atapoteza mechi zoote zikiwemo za majaribio. Tugange ijayo ili tuvuke hatua kwa hatua. Nawaza tu wala sijaanza kukulaumu ili na mimi nisije nikacheza 0/100.
 
Anatengeneza CV kupitia Tz,wakati anatutia aibu watu zaidi ya 55million,jana nilikuwa naangalia mpira na jamaa yangu ambaye anatoka kule mpira una weledi nilipata aibu sana,nilijaribu kumshawishi tutoke pale baada ya 45 minutes,akasema tumalizie kwanza.

Aliniuliza yaani timu yenu hata pasi tatu haipigi,halafu kocha amekaa tu.Aliendelea,hii ni mechi ya kirafiki kujaribu wachezaji mbona Kocha wa Egypt anafanya mabadiriko mapema wenu haoni hilo jambo.

Kutengeneza mfumo kipindi cha mashindano ni ngumu kufanikiwa,eti boko na Chilunda winger midfielders

Tukipata points hata tatu Afcon itakuwa maajabu ya soka
 
Well said bro!
 
K Kaka u-simba na U-Yanga vinasumbua sana vichwa vyetu. Kiujumla Jana timu ilicheza vizuri sana, mie nimeangalia mpira mwanza mwsho, Timu inacheza kwa pattern tofaout na wapondaji wanaosema eti butua butua. Acha hixo bwana, hata wamisiri kupata kigoli ilikuwa ni Nazi kwelikweli. Tupunguze ubinafsi ndg zangu na tuache kocha achague timu yake. Hao kina mkude unaowasifia ndiyo wanapigwaga mikono kila Mara (Ref. Algeria Vs Tz ) 7-0
 
watu mpira hamjui mnajifanya kujua,unaweza kushindana na misri kumiliki mpira kwa wachezaji wa kutoka hananasif,ambao njia za mpira wameenda kujifunza simba na yanga wakiwa tayari wameanza kunyoa ndevu!?
 
Erasto Nyoni pale nyuma hasa akitulia namba 6, ana mchango mkubwa sana. Viungo hawakuchangamka kabisa. Fei Toto si mchangamfu na hilo linafahamika. Himid Mao, nguvu nyingi bila sababu.

Pasi nyingi za timu yetu hazikuwa na macho kutokana na kukosa kujiamini. Nadhani Mudathir Yahya ndiye tegemeo pekee pale kati. Timu ilijilinda kwa dk zote 90 hivyo kufungwa kulikua hakuepukiki.
 
Una lessen ya ukocha lakin? We unafikiri rahis hivyo eti...
 
Achei ujuaji... hivi misri vs stars unataka maajabu gani?

Ila yule sijui anaitwa Warda wa misri ni hatari sana
 
Pressure yangu ni ya kushuka, siangaliagi mpira wa taifa staccmrs, nisije nikafa kizembe bure. Hadi nijishangae uko kaburini.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
kw mfumo wa Amunike M<chezaji pekee anayeweza kuonwa na mawakala atakuwa Aishi Manula kina Samatta hawawezi kuoneka sanasana atabebwa na sifa za Genk kwa viungo walishindwa kabisa kuicheza timu na kuchezesha washambulia, rafu za kijinga, kujilinda kama tuko ugenini tunatafuta pointi ya ugenini,
Kocha anatakiwa abadilike Msuva anatakiwa atokee pembeni sio kumweka katikati pamoja naa kujilinda hana plan hata za kufanya counter attack
 
nilisubiri nimwone yule mshambuliaji anayeongoza kwa magoli Uingereza lakini bado hata mabadiliko yaliyofanywa ni kuongeza ulinzi
 
Nilijiuliza sana kwa nini tulizidiwa pasi kiasikile, baada ya kusoma maoni ya wadau hapa nimeona kuwa Amunike ana sababu, hakutaka kuiweka timu mezani mwa adui zake, ile ni janja, kama Senegal kawaza kuwa ule ndo uwezo wetu amekwisha, Amunike ataipanga timu vzuri siku ya mashindano, tusubiri, mmeona mbali lakini Amunike kaona mbali zaidi, lakini pia nafkiri alitaka kujaribu mfumo wa kuzuia pale tunapozidiwa, kwa jana alifanikiwa ingawa sifa zimwendee kipa Aishi Manula, tuwe na subira wadau
 
mkuu umemaliza..kuna watu manyumbu sana...mtu hata kubetua mpira hawez ila anamponda amunike...nafkiri mwalimu alijaribu kufcha mbinu kwa wapinzani..na stratergy aliyotumia ya ku defence ni nzuri kwakua misri ni hatari..tunaweza tusifike mbali ila angalau tumetoa gundu
 
Tusibadili utaratibu....tutapata taabu sana...na tutajuta kwa nini tulienda huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…