Kwa mfumo wa ajira Tanzania, kujiajiri ukiwa umeajiriwa ni ngumu sana na kujiajiri ukiwa huna ajira ni ngumu zaidi! Nini kifanyike?

Kwa mfumo wa ajira Tanzania, kujiajiri ukiwa umeajiriwa ni ngumu sana na kujiajiri ukiwa huna ajira ni ngumu zaidi! Nini kifanyike?

Ndio maana Q-net wamewapiga wengi wamebaki wanahaha ngoja mie nibak kuuza tu simu zangu mpaka mzee baba atakapoondoka
 
Ndio maana Q-net wamewapiga wengi wamebaki wanahaha ngoja mie nibak kuuza tu simu zangu mpaka mzee baba atakapoondoka
Hao Q-Net wana dhambi sana wanawauzia watu saa tu million 5? aisee maneno mengi vitendo hakuna wasomi wanaungana kuwapiga ndugu zao sijapenda kabisa bora wangeungana wakafanya kitu kinachoonekana..
 
Hivi ni ipi hasa maana ya mafanikio katika haya maisha...?
Hakuna indication maalum ya mafanikio.
Kila binadam ana kitu chake au hali yake ambayo akiipata hiyo ndio inakuwa sehemu yake ya mafanikio.
Kuna mtu mafanikio yake ni kumiliki geto lenye kitanda,tv na sabufa.
Kuna mwingine mafanikio yake ni kumiliki gari,Kuna mwingine mafanikio yake ni kumiliki nyumba au kibanda,Kuna mwingine mafanikio yake ni kumiliki ghorofa,Kuna mwingine mafanikio yake ni kuwa mchamungu etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajamvi,

UTANGULIZI

Kwa asili ya ajira za kitanzania, ajira ambazo una uhakika wa kupata pesa ya kujikim ila sio ya ziada, ajira ambazo una uhakika wa kubanwa na kazi kwa masaa yote ya kazi, ajira ambazo zinagombaniwa na maelfu ya watu, etc kufikiria kujiajiri huku ukiwa umeajiriwa laweza kuwa bomu la kujilipua mwenyewe kama hukuwa makini.

Kwa asili ya hali za kibiashara Tanzania, ukiamua kujiajiri huku ukiwa huna sehemu unapopata kipato japo kidogo cha kujikimu cha kuajiriwa na ukaanza kuitegemea biashara changa ukilishe, ikuvishe, ikulipie pango, etc, basi kujiajiro huko kwaweza kuwa ni bomu zaidi ya lile la hapo juu.

NINI CHA KUFANYA?

1. Acha kuwaza biashara bali waza kupiga ela

Iwe umeajiriwa ama hujaajiriwa, uwe una mtaji ama huna mtaji jambo la kwanza unatakiwa kufanya ni kuachana na wazo la kuanzisha biashara badala yake anza kuwaza nawezaje kupiga ela. Nani ana ela niipige? Wapi pana ela nikaipige?

Tuelewane lakini sio kupiga ela kwa maana ya kupora, kuiba, kudhulumu, etc no sina maana hiyo. Zipo njia halali za kupiga ela ya mtu. Unamset fresh anaingia 18 zako unapiga ela.

2. Unaanzaje kupiga ela ya mtu huku akiwa amerizika kabisa wala hujamuibia na wala hujamzulumu?

a. Hatua ya kwanza ni kuchagua nani unataka upige ela yake?

b. Hatua ya pili ni kumchunguza anapendelea nini?

c. Hatua ya tatu ni kuchunguza je anapata kila anachotamani kukipata?

d. Hatua ya nne ni kuyaorodhesha yale ambayo unajua jamaa anayapenda ila hana pa kuyapata japo anayamudu.

e. Hatua ya tano ni kumset kwa nguvu kubwa ya ushawishi kuwa jambo flani linawezekana yeye tu akiamua.

f. Hatua ya sita ni kukomaa kumshawishi afanye jambo hilo.

g. Hatua ya saba ni wewe ku bridge the gap kati yake na jambo alipendalo kwa kumtoza pesa ama kwa kumuongezea bei.

ZINGATIA

Kukiwa na watu 10 ambao umepanga kupiga ela zao hao tunawaita leads.

Unaconvert leads ngapi kuwa pesa ni jambo la msingi. Jitaidi ukilenga watu kumi basi wanne usikose.

Ukiufanya huu mchezo kwa muda wa miezi kadhaa kwa mafanikio basi sasa upo tayari kuanza kufanya market research na kuamua biashara gani ya kufanya.

Biashara za kufanya watu hawatafuti mitandaoni kwa kusearch ama kwa kuuliza jf/fb/insta wala twitter. Wanazipata kwa kuwaza wapi pana ela nikapige.

Nawasilisha na nakaribisha michango yenu. Nakaribisha kukosolewa. Nakaribisha kupingwa. Nakaribisha kuungwa mkono. Ila plz sikaribishi matusi, dhihaka wala kejeli. Hapa ni Jamii Forums - The Home of Great Thinkers.

Courtesy of miamiatz
@Wewe miamiatz: na mwenzako @Cassanova69 Ni ma-jiniaz.


Ni wengi wenye Hela zao zikiwemo za mafao ya kustahafu, lakini mioyoni wana hofu ya Ku-invest kwenye kitu chochote, au ujuzi. Na wangetamani kufanya hivyo.

Ili Upige Pesa yao, Unakua ndio Superman wao, ukkwaongoza ku-Invest kwenye ndoto zao. Piga hela yao kupitia connections. Na vifaa wanavyoagiza.
Na ndio msingi wa kupata 'Business Idea' ya kwako binafsi. Itakayokufanya ujiajiri binafsi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom