Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Hata plate number kwa mara ya kwanza zimechelewa kubadilika, 2015 niliingiza gari nikapata number DCY mwaka wa 5 huu bado tupo kwenye D haijawahi tokea.

007 james Bond
Ofcourse hali ya uchumi inaweza kweli kuchangia kupungua kwa purchasing power, na hata kupelekea speed ya kuagiza magari kupungua kama ulivyodai, lkn hili la kutobadilika kwa plate number za magari, nafikiri linachangiwa na mabadiliko yalifanyika mwaka huo huo 2015, wa kutenganisha plate namba za magari na pikipiki na bajaj. Hii ikapelekea namba za magari ziende taratibu, hii psychologically imesaidia katika soka la magari used, mana zamani unakuta mtu anataka gari used ya mkononi lkn anatoa sharti lazima iwe namba 'C' ukimpelekea ya namba 'B' hata kama omenyooka kuliko 'C' atasita kununua.
 
You can’t teach an old dog a new trick.Hiyo ni miaka mingi sana kwenye biashara mkuu tena unaweza kuta wewe ni wale self employment(upo mwenyewe katika biashara hautaki hata msaidizi)akili imechoka hauna mbinu mpya tena.Get rest achia new generation waendeshe hiyo Biashara coz now days Biashara asilimia kubwa inafanyika online


iPhone 7plus
 
biashara za kuigana bongo nako zimezd kunaitaj ubunifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna biashara mpya wewe, kila biashara unayofikiria kufanya tayari ipo na ndio maana hizo bidhaa au huduma inapatikana. Kwani Kariakoo ni ya Juzi 2015? Au kuna siku miaka ya nyuma ulifika pale basi kila Duka ukakuta lina bidhaa tofauti na lingine? Ukiingia mtaa wa Hardware utakuta maduka yote ni ya Hardware, ukiingia mtaa wa Stationaries utakuta maduka yote ni ya stationaries na bidhaa zingine vivyo hivyo, hata Mwenge ukifika ule mtaa wakina mama wanaosuka nywele basi Frem almost zote pale ni salon na walikuwa wanafanya biashara vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo mwaka 2014 kurudi nyuma Kariakoo haikuwa na biashara nyingi za kufanana? Je kuna bidhaa zilizokuwa zinauzika vizuri kipindi cha nyuma ila kwasasa zimeachwa na wafanyabiashara wakaamua kuuza zinazofanana na jirani zao? Mnaongea kama mapunguani, Twende CHINA pale GUANGZHOU uangalie biashara hiyo kariakoo yenu nzima uichanganye na Lumumba na Posta haifikii eneo la soko la bidhaa Ya aina moja tu pale GUANGZOU.
Hapa kwetu tatizo uchumi wa mtu mmoja mmoja umeyumba hivyo kasi ya biashara imeshuka sana, na hapo ni wazi hutaweza kupata faida ya kulipa Kodi ya Pango wala ya Serikali (hata kama ni ileile uliyokuwa unalipa 2014) na hii inamaanisha hali itazidi kuwa mbaya zaidi kwakuwa uchumi ni mzunguko.
Kuna kitu kimoja ambacho wanaojiita wafanyabiashara hasa wa Dar ambacho hawakioni. Utitiri wa biashara za aina moja kwenye kila sehemu ya Dar nayo unachangia. Huwezi kuwa na jiji ambalo kila mtaa nyumba za barabarani wamejenga vibanda vidogo vidogo vinavyoita fremu na kwenye kila frem bidhaa ni za aina moja halafu utegemee biashara isifikie kwenye ''turning point'' siku moja. Jamani kama hiyo Kariakoo unayosema kila nyumba imegezwa ya biashara. Na mbaya zaidi nyumba moja imeganywa ''vichochoro'' vidogo vidogo vingi vinavyoitwa frem. Na kuweka chumvi kwenye kidonda bidhaa karibu zinafanana fanana. Hata Magufuli asingeingia madarakani nakuhakikishia hii hali lazima ingetokea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hardwares zipo busy, magari mapya tele mitaani, bar zinajaa pomoni

Wewe kama ilikuwa hulipi kodi kihalali ndio inakula kwako au kama biashara au wateja wako wengi wana linkage na zile sector zilizokua za kifisadi

Kuna biashara iliyokua maarufu nchi hii kama madawa ya kulevya? Viroba? Meno ya tembo? Wizi Bandarini? Wizi wa halmashauri? Sasa hayo mabilioni kwenye hayo maeneo ndio yalikua yanazagaa mitaani hovyo bila uchungu wala jasho, sasa hayapo tena lazima muone maisha hayaendi.

Mwandiko huu ni wa watu aina ya lemutuz,Hamna kazi ya maana wanafanya mjini zaidi ya dili na bashite wao, halafu wanakuwa na guts za kuwaambia wapambanaji ni wapiga dili. Subiri Magu aondoke aje mtaalamu wa kuset uchumi uone wanaume wanavyowapiga overtake kwa kupambania jasho lao halali mbwegeresi. Uchumi wa jumla unauliwa vinabaki vijitu vichache vinavyokula kipambe na visivyojua chochote vinakejeli watu na mitaji yao.
 
Kuna aina fulani ya biashara ambazo zimedorora kabisa, lakini zipo nyingine haziwezi kufa kabisa. Kila mtu lazima ale kwa hiyo biashara ya chakula haiwezi kufa kabisa ila badala ya kula mara tatu kwa siku watu watakula mara moja tu. Saluni za kina mama lazima ziwepo japo hela za kwenda saluni sasa zinapatikana kwa manati. Kwa ujumla biashara hapa nchini imeshuka sana kwa sababu mzunguko wa fedha umepungua.

Katika miaka iliyopita, matumizi ya serikali yalikuwa yanaachia pesa 'zishuke' kwa watu wa kawaida mitaani. Sasa hivi, serikali ina miradi mikubwa mikubwa (Steiglers, Standard Gauge, ununuzi wa ndege na flyovers) na miradi yote hiyo malipo yake yanaenda nchi za nje kwa sehemu kubwa kununua vifaa n.k. Zaidi ya hapo, miradi mingi ya serikali ilikuwa inafanywa na makampuni binafsi ambayo yalikuwa yanaajiri wananchi wa kawaida. Sasa miradi hii yote imepewa mashirika ya serikali (TBA, Suma JKT n.k.).

Kwa miaka miwili hivi iliyopita masoko ya mazao ya wakulima hayakuwa mazuri sana. Utakumbuka wanunuzi wa India walikataa kununua baadhi ya mazao yetu (ngwara, mbaazi n.k.). Baadhi ya wakulima waliuziwa mbegu na viuatilifu feki kwa hiyo hata uzalishaji ulishuka.

Wafanyabiashara waliokuwa wanakwepa kodi wamebanwa na TRA kwa hiyo wengi wamepunguza ukubwa wa biashara wanazofanya, na wengine (kwa mfano wale walio kwenye miji ya mipakani) wamehamishia biashara zao nchi jirani.

Kwa ujumla, mapato ya watu wa kawaida yamekuwa yanashuka. Na kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hii hali itaendelea. Tuombe Mungu mvua ambayo haina madhara inyeshe ili wakulima kila mahali nchini wavune vizuri. Kama hali ya chakula haitakuwa nzuri, sisi watu wa kawaida tutakuwa na shida kubwa sana.
.
 
Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku..
Tumeambiwa tupo pazuri. Tutembee kifua mbele. We are in da laiti tirak. Sasa hivi sisi ni dona kantri, tunatoa misaada Zimbabwe, Malawi na Mozambique
 
Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
Acha kulalamika mkuu
Funga hiyo biashara kama hailipi na wekeza kwenye kilimo cha Umwagiliaji!
Eg. mpunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom