Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Mkuu bora wewe bado unakomaa na biashara.. Wenzako tulishafunga muda mrefu, wanunuzi wako hoi na hawana pesa hizo bidhaa utamuuzia nani??

Kabla ya huyu jamaa nilikuwa nakuja dar kufunga mzigo kila mwezi, lakini alivyoanza sarakasi zake tu kila kitu kilikwenda kombo!!
 
Bandiko la maana sana hili na naunga mkono hoja,mtaani hali ni mbaya sana tunadumu kwa sababu ya uzoefu na kudra za Mungu tu kwamba biashara ametupa ndiyo vipawa vyetu tunavitumikia.

Ila mkuu believe me,utawala huu mfanyabiashara utakayefanikiwa ku-survive ukaenda na mchezo unavyotaka huko mbele hakuna kitakachokusumbua.tusisahau mfanyabiashara daily unajifunza kutokana na changamoto zilizo mbele yako na kadiri unavyozivuka ndivyo unavyozidi kujijengea mizizi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Kwa mtu ambaye hajawahi fanya biashara atakejeli ulichosema, ila kiuhalisia hali siyo kabisa. Kunasehemu ya biashara mahitaji ya nyumbani kipindi cha nyuma ilikuwa afadhali ila sasa kila anayepita anasema na kile nahitaji ila ngoja nitafute hela means uwezo wa kununua umepungua sana. Kusipokuwa na sababu na nia ya dhati ya kunusuru uchumi tutakwama.
 

Niko golini hapa toka saa mbili kamili asubuh mpaka sasa hv nna buku 7 tu dadeki utadhan mtoto wa lumumba.
 
Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
ukizoea kunyonga,kuchinja huwezi
Sasa ni kulipa kodi tu,kwa kua ulizoea kulipalaki tano kwa mwaka,lazima hali uone ngumu
 
Humu unataja unafanya biashara wakati watu wako frustrated na hiyo biashara mtu hajui hata ikoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu unataja unafanya biashara wakati watu wako frustrated na hiyo biashara mtu hajui hata ikoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunalalamika sisi ila kuna watu hata hawaelewi ukisema hiki kitu..Juzi kuna wateja wamekuja Kazini kwangu Madili ya hela waliyokua wanapiga Tena ni ya Halali kabisa wala sio wezi wala mafisadi Si ya kawaida watu wanapiga hela bwana..Nikasema Awamu hiii ina biashara na biashara na Mitaji na Mitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…