Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Biashara karibu zote tu, mi nipo kkoo mtu unawahi unafungua duka saa moja asubuhi, mpaka inafika saa nne hata mteja kuja angalau kuuliza bei tu hamna!
kwa kifupi uwezo wa watu kununua bidhaa umeshuka kwa kiasi kikubwa sana, tunasinzia tu madukani.

007 james Bond
Hali hiyo tunaoitia wengi,usikate tamaa,Ni mapito,neema zaja,huoni wa Monduli karudi nyumbani,mambo yatalegea kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli ukifanikiwa kutoboa awamu hii,hutakaa ufilisike tena kibiashara.Mambo yamekua hovyo biashara haipo kabsa,Wengi wamepoteza mitaji yao.Wafanyabiashara tuna hali ngumu sana[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata watumishi mirija imebanwa,waulize watakuhadithia,watu wa mtaani wanashabikia kufuata upepo ila Wote kwa pamoja tunaisoma 1,2,3,4,5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kimoja ambacho wanaojiita wafanyabiashara hasa wa Dar ambacho hawakioni. Utitiri wa biashara za aina moja kwenye kila sehemu ya Dar nayo unachangia. Huwezi kuwa na jiji ambalo kila mtaa nyumba za barabarani wamejenga vibanda vidogo vidogo vinavyoita fremu na kwenye kila frem bidhaa ni za aina moja halafu utegemee biashara isifikie kwenye ''turning point'' siku moja. Jamani kama hiyo Kariakoo unayosema kila nyumba imegezwa ya biashara. Na mbaya zaidi nyumba moja imeganywa ''vichochoro'' vidogo vidogo vingi vinavyoitwa frem. Na kuweka chumvi kwenye kidonda bidhaa karibu zinafanana fanana. Hata Magufuli asingeingia madarakani nakuhakikishia hii hali lazima ingetokea tu.
Sasa ulitaka kariakoo nyumba ziwe gest?
 
mmh.! unafanya biashara gani hiyo ambayo unapitia mabondeni na milimani.?
bila shaka we ni muuza dawa za kulevya au ndo wale wasiojulikana.

Mwingine huyu hapa. Watu ambao hawajawahi kufanya biashara ndio hao wanajipa utaalamu wa kutoa sababu ni kwa nini biashara za watu haziendi! Only in Tanzania you get this kind of idiocy.
 
Mwanangu pambana na hali yako. Siye mbele kwa mbele.
Kipindi hiki nimeweza kununua ndinga, kujenga house (siyo nyumba, namaanisha mjengo).
Nimepanda ndege
Nimefika uropa.

Hahahaha, awamu ya 5 ni zamu yetuuuuuuu
Itakuwa umeolewa na mumeo bado anayo pesa....ukiambiwa biashara zimebinuka elewa...no jokings hapa
 
Mkuu hata nikushukuru vipi kwa theard yako tumeshapiga kelele wanatuona wajinga hamna noma ngoja tusubiri October
 
Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
Sasa mbona mnajazana sana bar?! Hali kwenye mabar huwa haiakisi hali ngumu ya uchumi tuliyonayo.
 
Usiseme kwa sauti wasifia juhudi watakwambia tuko uchumi wa kati, na tumekuwa dona kantri zungumza chini chini hahahahahahah
 
Pole mwaya, tatizo serikali inafanya biashara na taasisi za serikali kwahyo kampuni nyingi binafsi ambazo zilikuwa suppliers wa serikali na walipa kodi wazuri zinakufa taratibu. Mungu akusaidie ila atusaidie na sisi maana cjui kama 2020 tutafika salama kama mambo yataendelea hivi.
Yaan acha tu. Mambo magumu mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa kabisa. Hta sisi biashara imefungwa siwezi kabisa kumlaumu bosi kwasababu hata mm ngekuwa nafasi yake ngefunga tu.

Na hamna dalili ya mambo kuwa mazuri
2014 nilikuwa na wafanyakaz karibia 50 ila sahiz wamebaki 21 na ntazid kupunguza hali ni mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom