SoC04 Kwa miaka 5-15 Tanzania tuwekeze katika kubadili fikra za watu kutoka walaji(consumers)kuwa wazalishaji(producers)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Fea_

New Member
Joined
May 23, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Mabadiliko Yote muhimu lazima yaanzie katika fikra na mtazamo.

Watanzania wengi tumekuwa na changamoto ya kuwa na fikra na mtazamo wa utegemezi kutoka mahali fulani.

Watoto wanakuzwa wakifundishwa kutegemea serikali kuwapatia kazi na maisha Bora.
Viongozi wanategemea nchi kuendelea kwa misaada kutoka kwa wahisani na nchi zilizoendelea.

Mitazamo na fikra kama hizi haziwezi kubadilisha maisha kwa namna yoyote kuanzia kwa mtu binafsi mpaka kwa Taifa zima.

Tunahitaji kuanza kuwafundisha vijana kuitegemeza jamii yao na Taifa kwa ujumla siyo kwa maneno au katika majukwaa bali katika programu maalumu ya miaka 5 hadi

Viongozi kuweka mikakati madhubuti namna ya nchi kuacha kuwa tegemezi kutoka kwa mataifa yalioendelea,hii haiondoi kuwa na mahusiano na mataifa mengine lakini mahusiano hayo yasiwe yakuinyonyaji(parasitic) kutoka kwa upande wowote

Tuko katika soko huria la ulimwengu mzima lililofunguliwa na teknolojia ya intaneti,lakini tanzania kutokana mifumo ya kiuongozi tumekuwa walaji zaidi ya wazalishaji jambo linalofanya tusinufaike zaidi na teknolojia hii leo watengeneza maudhui kupata malipo yao ni jambo gumu ukilinganisha na mataifa mengine yaliyoendelea.

Tunahitaji mabadiliko katika mtazamo wa jinsi tunavyotambua kusudi la kuwepo hapa duniani kila mmoja amekuja kwa kusudi la kufanya ulimwengu kuwa Bora,siyo kusubiri wengine wafanye ndipo sisi tufaidike.

Hata tupate teknolojia gani au tupewe kila kitu bado maisha hayatakuwa bora kama bado fikra hazijabadilika.Siyo ajabu leo kuona pesa za misaada zikitumika kinyume,ama miundombinu ikiharibiwa na wanafaika wenyewe.Tatizo hapo ni fikra na mitazamo mibaya kuhusu wajibu ni wa nani kufanya mambo yawe bora.

Hii ndiyo dawa endelevu la umaskini,kutojali au maumivu yanayowakuta wale wasijiweza,yule anayetegemewa anawaza na kumtegemea mwingine

Mazingira yanaharibiwa au kulindwa na wanaoyaishi,teknolojia hatutaweza kuifaidi kama mamlaka husika hazitaona wajibu wake wa kufanya mazingira kuwa rafiki kwa wale wanaowajibika kwao inasikitisha kuwa mitandao kama paypal katika nchi yetu huwezi kupokea pesa.

Mtazamo huu ninaouzungumza utakomboa sekta zote nchini kila mmoja atatimiza wajibu wake pale alipo na kwasababu tunategemeana kila mmoja maisha yatabadilika.

Hili litawezekana kwa kulifanya kampeni endelevu kwa kutoa elimu mashuleni,katika vyombo vya habari,nyumba za ibada na katika sehemu zote zenye mkusanyiko.Sera zitungwe za sheria pia zinazohimiza uwajibikaji na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji.
 
Upvote 4

Kweli mwanangu. Kila mmoja atimize kusudi lake kuifanya jamii kuwa bora zaidi.

Mtazamo huu ninaouzungumza utakomboa sekta zote nchini kila mmoja atatimiza wajibu wake pale alipo na kwasababu tunategemeana kila mmoja maisha yatabadilika.
Sawa kabisa
 
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom