Kwa Miaka 6 hatukuona wala kusikia ugonjwa wa Kipindupindu, hii ni aibu kwa Taifa

Kipindupindu kinafichika kweli???
Ni rahisi kuamini maneno ya unayemtaka kuliko unayemchukia.

  • Walisema kuhusu COVID19, Dunia imekataa
  • Kipindupindu kikifichwa na mamlaka, vifo vyake havitajidhihirisha kwenye jamii?
  • Ebola ikaze, mamlaka ifiche? Itaweza?

Nani anaweza thibitisha kuwa Mwele hakutumika?

Kwanini iwe rahisi kuamini intergrity ya mteuliwa kuliko mteuzi?

Nani yuko kwenye nafasi ya kupata taarifa sahihi kwa kulinganisha zaidi ya Raisi wa nchi?
 
Kwa maneno mengine tunatangaziwa kwamba watanganyika tunakulaga vinyesi!
 
Mbona mimi sina hiyo Taarfa ya kipindua pindua
 
Si kwamba hakukuwa na magonjwa wala njaa, vilikuwepo sana tu ila watu walilazimishwa kuficha taarifa makusudi na wao wakatii ili wasipoteze vibarua vyao.
Ina maama walipoambiwa kuficha taarifa hata majukwaa ya kijamii nayo yalikosa taarifa? Hata yule Kigogo aliyekua mtoa taarifa mkuu ?
Kuna vitu kuvificha haiwezekani ingejulikana tu.
 
Kilichomkuta Mwele ndio majibu sasa kwa nini hatukusikia mambo hayo wakatia wa Magufuli. Sayansi haikuwa na nafasi kwa Magufuli, ukweli haukuwa rafiki kwake. Rais Samia Suluhu anaruhusu ukweli usemwe kwenye mambo mengi.
Muhimu sana hapa ni kwamba kama mtoa mada anavyosema kwamba Kipindupindu ni ugonjwa wa aibu, baasi watu tuwe wasafi kuficha aibu hiyo. Huhitaji Rais mbabe kuwa msafi. Lets protect each other.
Swali la kujiuliza kama kweli ugonjwa huo wa Zika ulikuepo Tanzania baadaye uliishaje ?
Unataka kusema baada ya Dr. Mwele kutolewa na ugonjwa nao ukaogopa ukapotea ?
Magonjwa na majanga mbalimbali hayafichiki.
Magu pamoja na mapungufu yake yote ila kuna eneo alijitahidi.
Hivi COVID19 ingelipuka kipindi hiki si tungelazimishwa lock down. Ajabu ni kuwa ikifikia hapa watu wanakwepa kumpongeza jamaa
 
Hakuna neno zuri unaloweza kutumia zaidi ya aibu! Aibu! Aibu! tena aibu kubwa. Serikali kupitia Wizara ya afya imeutangazia Dunia hadharani kuwa ugonjwa wa kula kinyesi cha binadamu (kipindupindu) kimerejea nchini na tayari kuna wagonjwa 72 na 3 kati yao tayari wamekufa.

Kwamba ugonjwa huo uko maeneo mbalimbali nchini kama Katavi, Kigoma na Morogoro kwa maana unaendelea kusambaa. Kimsingi kwa lugha na maneno mepesi ni kwa kuugua kipindupindu ni kula kinyesi cha binadamu mwenzio kinacholetwa na nzi aliyetua kwenye kinyesi hicho na kisha kukileta kwako kupitia chakula chako ndipo unaanza kuharisha uharo mweupe kama uji wa mchele, kutapika, kuishiwa nguvu na kufa.

Hayati Magufuli alipoingia tu madarakani aliwatangazia maRC na maDC kwamba Wilaya au Mkoa wowote atakaposikia Kuna kipindu-pindu huyo DC au RC amejifukuzisha kazi. Matokeo yake Kwa miaka sita hatukusikia ugonjwa huu popote pale.

Vifo tulivyozoea kusikia kwa miaka hiyo sita ni watu kutekwa, kuteswa, kupotezwa, kuokotwa ndani ya sandarusi fukweni, Vifo vya presha kufuatia kupokonywa fedha zako kibabe kutoka benki na kila aina ya ukatili na udikteta na si kipindupindu.

Hebu tushirikiane kutokomeza kipindupindu kwa kuzingatia kanuni za usafi.

===

Waganga wakuu wa mikoa iliyotajwa kuwa na kipindupindu wamefunguka kuhusu kinachowasibu maeneo yao kutajwa kuwa na ugonjwa huo, huku ukosefu wa vyoo ukitajwa kuwa sababu kuu.

Juzi Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene alitangaza kuwa hadi Machi 11, 2023 Tanzania ilikuwa na wagonjwa wa kipindupindu 72, katika baadhi ya mikoa huku vifo vikiwa ni vitatu.

Hata hivyo, takwimu hizo huenda zikawa tofauti baada ya Mkoa wa Rukwa ulioripotiwa kuwa na wagonjwa 18 kukanusha kuwa hawana ugonjwa huo na taarifa kupelekwa wizarani lakini wanashangaa kusikia bado wamewekwa kwenye orodha.

Waziri Simbachawene alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa Mpango Shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu hadi ifikapo 2030, kwa kushirikisha wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na nje.

Baadhi ya mikoa iliyotajwa kuwa na wagonjwa ni Ruvuma 13, Kigoma saba, Katavi 34, na Rukwa wagonjwa 18 lakini Mkoa wa Manyara ulitajwa miongoni mwa iliyokuwa na wagonjwa pia.

Walichosema waganga wa mikoa
Akizungumza jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk Jesca Lebba alisema tatizo hilo lipo katika wilaya ya Uvinza na kwamba wamekuwa na mkakati wa namna ya kuondoa lakini kinachochangia ni kwa baadhi ya watu wenye utamaduni wa kutotumia vyoo.

Dk Lebba alisema eneo ambako kesi za kipindupindu zimeripotiwa, limekuwa mara kwa mara likikumbwa na ugonjwa huo, licha ya elimu na juhudi kubwa ambazo wameendelea kuzifanya ikiwemo kuhamasisha wananchi kuchimba vyoo na kuvitumia.

Alisema katika eneo hilo ndani ya wilaya ya Uvinza kuna kambi ambayo hawatumii vyoo na kwa hiyo idara yake ilishapeleka mapendekezo serikalini ili kuwaondoa wananchi na kufunga kambi hiyo kwa madai wahusika wanatakiwa kwenda kujifunza kwa wengine.

“Pale kuna kambi za watu ambao hawatumii vyoo kabisa, tumepeleka elimu na kuweka sheria kali lakini hakuna utekelezaji, sasa tumepeleka mapendekezo kwa mamlaka husika wawahamishe wananchi hao na kuzivunja kambi zao ili wakaishi kwa wengine wanaotumia vyoo,” alisema Dk Lebba.

Akizungumzia ugonjwa huo katika Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Mkoa huo, Queen Sendiga alisema hatambui kama mkoani kwake kuna wagonjwa au matukio ya ugonjwa huo, huku akimtaka mwandishi kuwasiliana na mganga mkuu wa mkoa huo.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dk Ibrahimu Mwita, alishangazwa kusikia mkoa wake ukiendelea kutajwa wakati alishatoa taarifa wizarani siku nyingi kwamba hakuna sampuli zilizoonyesha kwamba mkoa huo una wagonjwa.

Dk Mwita alisema awali kulikuwa na watu waliohisiwa lakini walipochukua sampuli za vipimo na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu, majibu yalitoka kuwa hakuna ugonjwa huo ndipo akaiandikia wizara na hadi sasa hawana wagonjwa, huku akiomba mkoa huo uongolewe kwenye orodha.

“Sisi hatuna kipindupindu na wala hatukuwahi kuwa nacho niliwaandikia wizara baada ya kufuatilia maeneo yote lakini nashangaa kwa nini hadi leo tunatajwa tena kwamba ni miongoni mwa mikoa yenye shida ya kipindupindu tena, tutawaomba watuondoe,” alisema Dk Mwita.

Katika taarifa ya Waziri Simbachawene ambayo imesambazwa katika vyombo vya habari, moja ya changamoto katika ugonjwa huo ni ukosefu wa maji safi na salama, uelewa mdogo wa namna ya kupambana na kipindupindu,jamii kukosa vyoo bora na matumizi sahihi ya vyoo hivyo.

Simbachawene alisema hadi kufikia Machi mwaka huu nchi ya Malawi ilikuwa na jumla ya wagonjwa 52,167 na vifo 1620 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alisema taarifa hiyo inatoa tahadhari ya uwezekano wa ugonjwa huo kuvuka mipaka na kuingia nchini.

Kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel alisema, wizara ya afya imejipanga katika hospital za kanda,mkoa hadi ngazi ya zahanati ili kuhakikisha inajikinga na kutokomeza ugonjwa huo.

Mwakilishi wa Shirika la Save the Children Angela Kauleni alisema shirika hilo liko tayari kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo, huku akisisitiza kuwa elimu ya matumizi ya vyoo bado ni changamoto kwa wananchi.

Chanzo: Mwananchi

Nenda kamfufue siku ya tarehe 9/4/2023 ili mkale pamoja paska.
wasukuma ni washamba sana hivi mtu amekufa kaoza miaka miwili sasa bado mna imani za gambushi, sasahivi yuko mama Samia na post zote mlizokuwa mmejimegea na yule dikteta zimegawanywa sawa na liuwanja lenu chato litabaki na mapanya na majoka
 
Swali la kujiuliza kama kweli ugonjwa huo wa Zika ulikuepo Tanzania baadaye uliishaje ?
Unataka kusema baada ya Dr. Mwele kutolewa na ugonjwa nao ukaogopa ukapotea ?
Magonjwa na majanga mbalimbali hayafichiki.
Magu pamoja na mapungufu yake yote ila kuna eneo alijitahidi.
Hivi COVID19 ingelipuka kipindi hiki si tungelazimishwa lock down. Ajabu ni kuwa ikifikia hapa watu wanakwepa kumpongeza jamaa
Haters gonna hate hata iweje !!
 
Ni rahisi kuamini maneno ya unayemtaka kuliko unayemchukia.

  • Walisema kuhusu COVID19, Dunia imekataa
  • Kipindupindu kikifichwa na mamlaka, vifo vyake havitajidhihirisha kwenye jamii?
  • Ebola ikaze, mamlaka ifiche? Itaweza?

Nani anaweza thibitisha kuwa Mwele hakutumika?

Kwanini iwe rahisi kuamini intergrity ya mteuliwa kuliko mteuzi?

Nani yuko kwenye nafasi ya kupata taarifa sahihi kwa kulinganisha zaidi ya Raisi wa nchi?
Na ajabu baada ya Mwele kutimuliwa Zika nayo ikaondoka naye !!
 
Hakuna neno zuri unaloweza kutumia zaidi ya aibu! Aibu! Aibu! tena aibu kubwa. Serikali kupitia Wizara ya afya imeutangazia Dunia hadharani kuwa ugonjwa wa kula kinyesi cha binadamu (kipindupindu) kimerejea nchini na tayari kuna wagonjwa 72 na 3 kati yao tayari wamekufa.

Kwamba ugonjwa huo uko maeneo mbalimbali nchini kama Katavi, Kigoma na Morogoro kwa maana unaendelea kusambaa. Kimsingi kwa lugha na maneno mepesi ni kwa kuugua kipindupindu ni kula kinyesi cha binadamu mwenzio kinacholetwa na nzi aliyetua kwenye kinyesi hicho na kisha kukileta kwako kupitia chakula chako ndipo unaanza kuharisha uharo mweupe kama uji wa mchele, kutapika, kuishiwa nguvu na kufa.

Hayati Magufuli alipoingia tu madarakani aliwatangazia maRC na maDC kwamba Wilaya au Mkoa wowote atakaposikia Kuna kipindu-pindu huyo DC au RC amejifukuzisha kazi. Matokeo yake Kwa miaka sita hatukusikia ugonjwa huu popote pale.

Vifo tulivyozoea kusikia kwa miaka hiyo sita ni watu kutekwa, kuteswa, kupotezwa, kuokotwa ndani ya sandarusi fukweni, Vifo vya presha kufuatia kupokonywa fedha zako kibabe kutoka benki na kila aina ya ukatili na udikteta na si kipindupindu.

Hebu tushirikiane kutokomeza kipindupindu kwa kuzingatia kanuni za usafi.

===

Waganga wakuu wa mikoa iliyotajwa kuwa na kipindupindu wamefunguka kuhusu kinachowasibu maeneo yao kutajwa kuwa na ugonjwa huo, huku ukosefu wa vyoo ukitajwa kuwa sababu kuu.

Juzi Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene alitangaza kuwa hadi Machi 11, 2023 Tanzania ilikuwa na wagonjwa wa kipindupindu 72, katika baadhi ya mikoa huku vifo vikiwa ni vitatu.

Hata hivyo, takwimu hizo huenda zikawa tofauti baada ya Mkoa wa Rukwa ulioripotiwa kuwa na wagonjwa 18 kukanusha kuwa hawana ugonjwa huo na taarifa kupelekwa wizarani lakini wanashangaa kusikia bado wamewekwa kwenye orodha.

Waziri Simbachawene alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa Mpango Shirikishi wa Taifa wa kuzuia na kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu hadi ifikapo 2030, kwa kushirikisha wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na nje.

Baadhi ya mikoa iliyotajwa kuwa na wagonjwa ni Ruvuma 13, Kigoma saba, Katavi 34, na Rukwa wagonjwa 18 lakini Mkoa wa Manyara ulitajwa miongoni mwa iliyokuwa na wagonjwa pia.

Walichosema waganga wa mikoa
Akizungumza jana, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk Jesca Lebba alisema tatizo hilo lipo katika wilaya ya Uvinza na kwamba wamekuwa na mkakati wa namna ya kuondoa lakini kinachochangia ni kwa baadhi ya watu wenye utamaduni wa kutotumia vyoo.

Dk Lebba alisema eneo ambako kesi za kipindupindu zimeripotiwa, limekuwa mara kwa mara likikumbwa na ugonjwa huo, licha ya elimu na juhudi kubwa ambazo wameendelea kuzifanya ikiwemo kuhamasisha wananchi kuchimba vyoo na kuvitumia.

Alisema katika eneo hilo ndani ya wilaya ya Uvinza kuna kambi ambayo hawatumii vyoo na kwa hiyo idara yake ilishapeleka mapendekezo serikalini ili kuwaondoa wananchi na kufunga kambi hiyo kwa madai wahusika wanatakiwa kwenda kujifunza kwa wengine.

“Pale kuna kambi za watu ambao hawatumii vyoo kabisa, tumepeleka elimu na kuweka sheria kali lakini hakuna utekelezaji, sasa tumepeleka mapendekezo kwa mamlaka husika wawahamishe wananchi hao na kuzivunja kambi zao ili wakaishi kwa wengine wanaotumia vyoo,” alisema Dk Lebba.

Akizungumzia ugonjwa huo katika Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Mkoa huo, Queen Sendiga alisema hatambui kama mkoani kwake kuna wagonjwa au matukio ya ugonjwa huo, huku akimtaka mwandishi kuwasiliana na mganga mkuu wa mkoa huo.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dk Ibrahimu Mwita, alishangazwa kusikia mkoa wake ukiendelea kutajwa wakati alishatoa taarifa wizarani siku nyingi kwamba hakuna sampuli zilizoonyesha kwamba mkoa huo una wagonjwa.

Dk Mwita alisema awali kulikuwa na watu waliohisiwa lakini walipochukua sampuli za vipimo na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu, majibu yalitoka kuwa hakuna ugonjwa huo ndipo akaiandikia wizara na hadi sasa hawana wagonjwa, huku akiomba mkoa huo uongolewe kwenye orodha.

“Sisi hatuna kipindupindu na wala hatukuwahi kuwa nacho niliwaandikia wizara baada ya kufuatilia maeneo yote lakini nashangaa kwa nini hadi leo tunatajwa tena kwamba ni miongoni mwa mikoa yenye shida ya kipindupindu tena, tutawaomba watuondoe,” alisema Dk Mwita.

Katika taarifa ya Waziri Simbachawene ambayo imesambazwa katika vyombo vya habari, moja ya changamoto katika ugonjwa huo ni ukosefu wa maji safi na salama, uelewa mdogo wa namna ya kupambana na kipindupindu,jamii kukosa vyoo bora na matumizi sahihi ya vyoo hivyo.

Simbachawene alisema hadi kufikia Machi mwaka huu nchi ya Malawi ilikuwa na jumla ya wagonjwa 52,167 na vifo 1620 kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alisema taarifa hiyo inatoa tahadhari ya uwezekano wa ugonjwa huo kuvuka mipaka na kuingia nchini.

Kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel alisema, wizara ya afya imejipanga katika hospital za kanda,mkoa hadi ngazi ya zahanati ili kuhakikisha inajikinga na kutokomeza ugonjwa huo.

Mwakilishi wa Shirika la Save the Children Angela Kauleni alisema shirika hilo liko tayari kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo, huku akisisitiza kuwa elimu ya matumizi ya vyoo bado ni changamoto kwa wananchi.

Chanzo: Mwananchi
Yule Dikteta sio tu alikuwa akiteka na kuus watu, bali hata mlipuko wa magonjwa mengi alikuwa akificha
Mfano Ugonjwa wa Covid ambao ulimuondoa hadi Katibu Mkuu Kiongozi, kabla ya kunuondoa yeye alikuwa akikataa na kuuita matatizo ya kupumua
 
Si kwamba hakukuwa na magonjwa wala njaa, vilikuwepo sana tu ila watu walilazimishwa kuficha taarifa makusudi na wao wakatii ili wasipoteze vibarua vyao.
Acha uongo wewe.mngeshindwa kimtumia kigogo,ambaye mlimtumia adi vifo hewa vya corona
 
Hayati Magufuli alipoingia tu madarakani aliwatangazia maRC na maDC kwamba Wilaya au Mkoa wowote atakaposikia Kuna kipindu-pindu huyo DC au RC amejifukuzisha kazi. Matokeo yake Kwa miaka sita hatukusikia ugonjwa huu popote pale.
Wewe ukishatangaziwa kuwa utafukuzwa kazi kipindupindu kikisikika mkoani pako si unajua cha kufanya hata kama ugonjwa huo upo?
 
Vifo huwezi kuvificha kama vinatokea ! Hata kwenye corona japo vilikuwa havitangazwi lakini vifo vya corona vilikuwa vinajulikana kila vinapotokea !! Haters gonna hate hata iweje !!
 
Back
Top Bottom