Kwa Million 15 Kushuka chini, naweza kupata Gari kutoka Japan?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Habari za mishe mishe wakuu.

Kila mtu anatamani harufu ya gari kutoka Japan. Tatizo linaweza kuja kwenye budget. Sasa tu-assume tuna maximum budget ya Mil 15 tu, je tunaweza kupata gari kutoka JP?

Magari ya Million 15 na kushuka chini

1. Honda Fit (2nd gen, 2007 -2012)

Unaweza ukapata hii gari kutoka Honda, kwa bei nzuri kutoka JP. Mfano, JP unaweza ukapata Honda Fit ya grade 3.5 kwenda juu kuanzia Tsh Mil 6.5 tu.

Ushuru wa hii gari ni Mil 5.6 hadi Mil 6 (factors zipo nyingi).

Honda Fit ni moja ya gari nzuri sana, na ina option ya Fit RS (Sport) ambayo uta enjoy sana.


2. Suzuki Swift (1st & 2nd gen, 2004 - 2009, 2010 - 2015)

Unaweza ukajipatia Suzuki Swift (na Swift Sport of course) kwa bei rafiki chini ya Mil 15. Hapa una options ya 1st gen na 2nd gen.

Unaweza ukapata hizi gari kwa Mil 7 kushuka chini kwenye website za kuagiza magari JP.

Na ukalipia Ushuru wa kuanzia Mil 5.5 kwa 1st gens au hadi Mil 7 kwa kuzingatia mwaka na vigezo vingine.

Hapo hapo kwenye Suzuki, unaweza kucheki na Suzuki Alto kama bonus point.

3. Mazda Demio (2nd gen & 3rd gen, 2002 - 07, 2008 - 2013)

Mazda anatengeneza gari nzuri sana, kwa bei rafiki. Kuna hii gari inaitwa Mazda Demio kali sana kwa bei rafiki.


Mfano hiyo juu ni 2nd gen ya 2008 unaweza ipata kwa Mil 6 hivi na ushuru Mil 5.5 hivi.


Na bado ukijitanua ukachukua 3rd gen, utapata kwa bei iyo iyo tu 6-7 Mil.


Ushuru wakw nayo sio mkali ni Mil 6 kasoro kidogo. Mfano hiyo ya juu ya 2014 ushuru Mil 6 tu kama inavyoonekana kwenye calculator ya TRA hapa chini.

Bonus ya Mazda naomba nikupe Mazda Verisa, nae tunampata kwa bei chee, Mil 6 kushuka chini na ushuru Mil 6 kushuka chini.


4. Honda Insight (2nd gen, 2009 - 2016)

Twende Hybrid sasa. Honda Insight. Hii ni Hybrid kutoka Honda inayoshindana na Toyota Prius.


Muonekano ni subjective, ila mi naionaga imekaa poa. Kwenye mafuta inanusa, kwasababu ni Hybrid.

Unaweza ipata kati ya Mil 6 hadi 7 JP na TRA watataka Mil 6 na kuendelea kutokana na vigezo vyao.

Mfano, hii hapo juu ni ya 2009 kwa Mil 6.1 sio mbaya kabisa.

5. Suzuki Carry (9th gen, 1991 - 1999)

Kwa wapanbanaji, unaweza nunua Suzuki Carry kwaajili ya mishe mishe. Hivi vi gari vitakuingizia hela siku kwa siku, na bei yake ni ndogo sana huwezi amini.

Nyingi zinauzwa kwa bei kuanzia Mil 5 na kuendelea. Mfano hii ya 1993 Mil 5 bila kunegotiate.


Mfano, hii hapa ya mwaka 1993 TRA wanataka Mil 4.7 tu.


Kwahiyo ukitulia ukafanya research, utapata Carry nzuri tu.

Mengineyo:

Honda Stream



Subaru Impreza


Mazda Axela Sport


Nissan Note


Toyota Belta

Tunaweza kuongeza na mengine, kwa kuzingatia CIF na ushuru wa TRA.

PAMOJA
 
Bila kusahau mazda verisa, honda freed & freed spike....Na nyengine nyingi brand nje ya toyota.. mchawi spare maana unaweza kuta dar nzima unaimiliki peke yako
 
Hivyo ni vyombo vya usafiri tu kama punda, farasi, guta, bajaji na boda boda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…