Kwa mkataba huu mpya wa Pique Barcelona klabu gani itaweza kumnunua?

ilejehome

Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
22
Reaction score
17


Beki wa klabu ya Barcelona Gerard Pique amesaini mkataba mpya ambao utamuweka kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2022.

Lakini moja kati ya vitu vikubwa ambavyo vipo kwenye mkataba wa nyota huyo ni kipengele kinachoitwa buy-out clause yenye thamani ya €500million (£441million). Hii ina maana kuwa endapo klabu yoyote itahitaji kumsajili akiwa ndani ya mkataba itatakiwa kulipa hiyo pesa iliyopo kwenye buy-out clause.

Klabu gani itathubutu kumsajili?
 
Hao ndiyo wazungu wanajua biashara..

Bongo mkataba miaka 2 halafu mwisho wa siku mtu anaondoka free kama Ajibu vile
 
kwa buy out clause hiyo na ukitazama umri wa pique nakuwa na shaka na thamani yake.
 
Pique ni beki wa kawaida sana kwa sasa yaani hata wasingeweka dau hilo sidhani kama thaman yake inazidi p25. Pique kwa sasa ukimpeleka vilabu kama Man u, man city, Chelsea & PSG atakaa bench hapati no ya moja kwa moja
 
Pique ni beki wa kawaida sana kwa sasa yaani hata wasingeweka dau hilo sidhani kama thaman yake inazidi p25. Pique kwa sasa ukimpeleka vilabu kama Man u, man city, Chelsea & PSG atakaa bench hapati no ya moja kwa moja
Hayo ni mawazo yako,,ila usifikiri kama wazungu hawana akili,,kuna kitu wanakitaka kwa Pique zaidi hata ya mchezo wenyewe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…