Beki wa klabu ya Barcelona Gerard Pique amesaini mkataba mpya ambao utamuweka kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2022.
Lakini moja kati ya vitu vikubwa ambavyo vipo kwenye mkataba wa nyota huyo ni kipengele kinachoitwa buy-out clause yenye thamani ya €500million (£441million). Hii ina maana kuwa endapo klabu yoyote itahitaji kumsajili akiwa ndani ya mkataba itatakiwa kulipa hiyo pesa iliyopo kwenye buy-out clause.
Klabu gani itathubutu kumsajili?