sanalii
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,639
- 5,767
Harakati za hela ya umeme nyumba za kupanga zenye kushare Luku.
Few years ago, nilipanga chumba, wapangaji tulikua wawili na mtoto wa mwenye nyumba, kwakua mtoto wa mwenye nyumba alikua anatatizo la akili, tulimtoa katika kuchangia umeme, pia hakua na matumizi makubwa.
Mwanzoni mambo yakawa sawa, ila muda ulivyozidi, ikifika zamu ya mwenzangu anasema hana hela tunalala giza, nami nilikua nasoma hivyo ilinilazimu ninunue tu umeme.
Nikawaza emotional energy ninayotumia kumfikiria huyu mpangaji mwenza, nikaona bora tu niwe nalipa mwenyewe, after all, yeye pia hakua na matumizi makubwa zaidi ya taa tu na kuchaji simu, nililipa umeme pekeangu kwa miezi kama mitano.
Mtoto wa mpangaji akaondoka kutokana na tatizo la akili kuzidi, hivyo chumba wakaweka mpangaji mwengine.
Mpangaji wa tatu alipofika, akawa yeye feni anawasha saa moja jioni anazima saa mbili asubuhi, binafsi nikaona siwezi tena kugharamia umeme pekeangu, ikabidi tuitane tuchangie wote, mpangaji mgeni alikua ana kama wiki hivi, jamaa alitoa hela ila kumbe kile kitendo kimemuuma kua ni kama tumemhusisha na umeme mapema,
Kisanga sasa:-
Akawa anawasha feni na taa masaa 24, yani anaweza kutoka akaacha vyote vinawaka makusudi, feni zilikua ni zile za zamani zinakula sana umeme.
Jinsi ya kumwambia ni ngumu mana atasema na yeye amechanga, hakika hii ilikua moja ya sababu ya kuhama.
Kuna watu ni kiburi na usiombe ukutane nae maeneo ambayo huwezi muepuka