Kwa mpango huu nini hatima ya TRA juu ya biashara yangu

fizo talent

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
2,255
Reaction score
3,889
Kwenye mwezi wa tatu mwaka huu baada ya kujimeki sana niliamua kufungua biashara fulani baada ya vyuma kukaza sana.
Ila changamoto ikaja baada ya kuanza bishara eneo nililopo ikawa tra kila iitwayo leo lazima watie tim kiasi kwamba nililazimika niwe nafunga hali iliyopelekea maisha yazidi kua magumu zaidi na hapo ukizingatia hela yote niliyonayo niliingiza ktk biashara.
Nikaamua nifatilie tin ikiwezekana na hata leseni ili niweze kupambana na hali yangu vizuri ila nilipoenda tra ndipo nilipochoka maana msingi wangu ulikua ni laki 7 na wao wakanikadiria nilipe laki 6 na 20 na senti kadhaa kwa mwaka na wakanipa document zao kiasi ambacho inabidi nilipe kwanza baada ya kugawa huo mwaka kua kila baada ya miezi mitatu nikalipe,kwa awamu ya kwanza ilibidi nilipe laki mbili na mashilingi kibao kitu ambacho kwangu ulikua mlima mrefu nisioweza kuupanda.

Mwisho wa siku niliamua kuendelea na biashara maana sikua na namna nyingine ya kuniingizia kipato,biashara iliendelea japo kwa kukimbizana sana na tra kila ukiskia wanakuja ilinibidi nifunge ili kuepusha shari.Baada ya kukomaa sana kwa takribani miezi nane sasa nataka nifatilie tena ili niweze kupata tin na leseni yake.
Hapa ndipo ninapotaka kujua je?nikijepeleka na kusema nilikuja ila sikurudi tena kwa kua documents bado ninazo si nitalundikiwa mikodi kibaaao na penat za kutosha kiasi nitashindwa kumudu kulipa na je? ni vp nikisema nianze process upya si nitagundulika maana kule hadi picha nilipigwa kipindi kile nilivyofuatilia kabla ya kula chochoro kwa kipindi chote hiki.

Nawasilisha na pia msaada kwa mjuvi wa haya mambo
 
Kuomba ushaur wa jins ya kukwepa kodi ni kosa la jinai, usituingize hatiani, lipa kodi uliokadiriwa uendellee na biashara yako! Au kuwa jingaazi rais wenu anawabeba!
 
Kuomba ushaur wa jins ya kukwepa kodi ni kosa la jinai, usituingize hatiani, lipa kodi uliokadiriwa uendellee na biashara yako! Au kuwa jingaazi rais wenu anawabeba!
Sio kukwepa mkuu shida inakua kwenye makadirio km mimi nilikadiriwa kikubwa mpaka nikashindwa kulipa
 
Pole sana, mimi huu mwaka wa 8 sijawahi lipa kodi
Ila next year lazima nilipe, jaribu kupata ushauri kwa wale wanaosadia kusajili kampuni
 
Pambana nao.
Hao watu Kama wewe. Wakishindwa kukuelewa waache wafunge biashara. Sasa hapo si utakuwa unawatafutia wao washibe matumbo Yao wakati wewe unaumia. KAZA.
 
Jitahidi usifanye biashara rasmi,hii serikali inataka watu wasiweke hela benki au ujenge jengo lenye kuonekana,hivyo ukiwa na biashara rasmi itakula kwako nafuu uwe machinga na usilipe kodi,ukiwa na hela isiende benki watafuata huko hivi karibuni.
 
Kwa benki sipo kabisa ila hapo kwenye biashara isiyo rasmi ndio majanga maana sio machinga ila kwa mjasiria mali mdogo hizi ni changamoto kubwa sana
 
Pambana nao.
Hao watu Kama wewe. Wakishindwa kukuelewa waache wafunge biashara. Sasa hapo si utakuwa unawatafutia wao washibe matumbo Yao wakati wewe unaumia. KAZA.
Shida ya huu mpambano mimi nimeshika kwenye makali na ukisema uwaache wafunge biashara naona hasara itakua upande wangu zaidi kuliko kwao
 
Kikubwa kawaone mkuu rudi TRA au tafuta consultant muulize ila nijuavyo utabaki pale pale penat ni kidogo maana unahesabika mkwepa kodi punguza woga mjasiriamali HAOGOPI
HUMU UTAWAPATA WATUMWA WENGI hawana ushauri
 
Asante kwa ushauri wako wa ujasiri
 
Shida ya huu mpambano mimi nimeshika kwenye makali na ukisema uwaache wafunge biashara naona hasara itakua upande wangu zaidi kuliko kwao
Hawawezi kufunga.
Wakifunga wapeleke mahakamani.
Acha uoga. Pambana nao. Waambie napenda kulipa kodi. Ila makadirio yenu ya kodi ni makubwa kwangu. Tukaeni tufanye tena tathmini.
UKIONA WANAZINGUA WAAMBIE NATAKA KULIPA KODI KWA MFUMO WA EFDS.
WAKIKUPA AKILI KICHWANI KWAKO. [emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…