Kwenye mwezi wa tatu mwaka huu baada ya kujimeki sana niliamua kufungua biashara fulani baada ya vyuma kukaza sana.
Ila changamoto ikaja baada ya kuanza bishara eneo nililopo ikawa tra kila iitwayo leo lazima watie tim kiasi kwamba nililazimika niwe nafunga hali iliyopelekea maisha yazidi kua magumu zaidi na hapo ukizingatia hela yote niliyonayo niliingiza ktk biashara.
Nikaamua nifatilie tin ikiwezekana na hata leseni ili niweze kupambana na hali yangu vizuri ila nilipoenda tra ndipo nilipochoka maana msingi wangu ulikua ni laki 7 na wao wakanikadiria nilipe laki 6 na 20 na senti kadhaa kwa mwaka na wakanipa document zao kiasi ambacho inabidi nilipe kwanza baada ya kugawa huo mwaka kua kila baada ya miezi mitatu nikalipe,kwa awamu ya kwanza ilibidi nilipe laki mbili na mashilingi kibao kitu ambacho kwangu ulikua mlima mrefu nisioweza kuupanda.
Mwisho wa siku niliamua kuendelea na biashara maana sikua na namna nyingine ya kuniingizia kipato,biashara iliendelea japo kwa kukimbizana sana na tra kila ukiskia wanakuja ilinibidi nifunge ili kuepusha shari.Baada ya kukomaa sana kwa takribani miezi nane sasa nataka nifatilie tena ili niweze kupata tin na leseni yake.
Hapa ndipo ninapotaka kujua je?nikijepeleka na kusema nilikuja ila sikurudi tena kwa kua documents bado ninazo si nitalundikiwa mikodi kibaaao na penat za kutosha kiasi nitashindwa kumudu kulipa na je? ni vp nikisema nianze process upya si nitagundulika maana kule hadi picha nilipigwa kipindi kile nilivyofuatilia kabla ya kula chochoro kwa kipindi chote hiki.
Nawasilisha na pia msaada kwa mjuvi wa haya mambo