Kwa mpango huu nini hatima ya TRA juu ya biashara yangu

Pamoja mkuu
 
Kama unahitaji msaada wowote kuhusiana na mambo ya kodi za TRA nicheki PM mkuu
 
Sio kukwepa mkuu shida inakua kwenye makadirio km mimi nilikadiriwa kikubwa mpaka nikashindwa kulipa
Yaani kama ulishaingia kwenye system jitahidi tu ulipe kadri unavyochelewa deni linaongezeka...lipa kodi kwa maendeleo ya nchi
 
Pole sana mkuu
Anyway nicheki hapa email:iconsultbuzness@gmail. com! Hotline: 0659211222\0777 777 766
 
Sijui utaratibu wa kodi upoje mtaji laki 7 kodi laki 6
Mtaji wa lakini 7 (kama huuzi madawa ya kulevya) ni mdogo mno hata faida unayopata haistahili kulipiwa kodi. Unapaswa kujiandikisha kama mlipa kodi (TIN) na unapaswa kupeleka taarifa (return) kila baada ya miezi mitatu. Katika hiyo return unajikadilia faida utakayopata ambayo ndiyo inalipiwa kodi. Kwa kiwango chako cha mtaji nahisi faida yako itakuwa ndogo na hivyo kuwa nje ya wigo wa kutozwa kodi. Kuwa na leseni ni lazima lakini unaipata baada ya kumalizana na TRA.
 
Shida ya huu mpambano mimi nimeshika kwenye makali na ukisema uwaache wafunge biashara naona hasara itakua upande wangu zaidi kuliko kwao
Kama hujawahi kupeleka maombi ya TIN, yaani huna failing TRA, nenda kama vile unataka kuanza biashara. Labda awepo mtu anayejua kuwa unayo biashara tayari. Vinginevyo anza upya. Watu wa TRA wanakadiria kodi kubwa wakiona huna uelewa wa kutosha na mambo ya kodi. Pata msaada/ushauri wa kitaalamu. Utaulipia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…