Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Israel inaposhangilia kuokolewa kwa mateka 4 huku 4 wengine wakishindikana na kufa pamoja na raia 274 ni tangazo la kusema vita dhidi ya Hamas ni vigumu mno.
Mateka hao wamepatikana kwa msaada wa askari wa Marekani waliopo Gaza na wenzao wa kiyahudi waliojifanya kama wahamiaji kutoka Rafah,
Katika tangazo lao kwenye chaneli ya telegram,Hamas wamekiri kuponyokwa na mateka hao wanne lakini wakasema mateka wengine wanne akiwemo mmoja mmarekani wameuliwa katika purukushani hizo za uokoaji.
Kwa upande wake mshauri wa masuala ya kiulinzi wa Marekani,Jake Sullivan amethibitisha kuwa kweli Marekani imehusika na uokoaji huo bila kutaka kujadili zaidi uhusika wao.
Matukio hayo yametokea kwenye kambi ya Nusreita ili katikati ya Gaza ikiwa ni karibu mwezi wa 9 tangu vita vianze baina ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hamas na makundi mengine ndani ya Gazi.
Mataifa mengi duniani kwa mara nyengine yamelaani mauwaji hayo ya idadi kubwa ya watu kwa ajili ya kuokoa mateka 4 wakati juhudi za kusimamisha vita zikiwa zimekwamishwa na ukaidi wa serikali ya Benjamin Netanyahu na baraza lake la vita.