Kwa mshahara huu, naweza kupata mkopo kiasi gani?

Alichosema dist111 ni sahihi ila huyu anayesema Equity Bank itakupa milioni zote hizo sio kweli hata kidogo..na haitakaa itokee!

Hesabu ziko hivi:

Let'a say riba ni 18% kwa mwaka..chukulia unakopa tsh 9,000,000/=

Fanya 9,000,000 x 18% = 1,620,000 hii ndiyo faida yao wanayokukata kwa mwaka.
Sasa kwa miaka mitano itakuwa 1,620,000 x 5 = 8,100,000 kama riba.
Kwa hiyo sasa,jumla ya pesa yote utakayolipa ni riba + mkopo wenyewe: 8,100,000 + 9,000,000 = 17,100,000/=

So,ili kujiua kwa mwezi utakatwa sh ngapi: 17,100,000 gawa kwa miezi ya miaka mitano(miezi 60) = 285,000/=

Kimsingi hela unayolipa hadi mkopo unakwisha ni kubwa sana kama unaichukulia kama ilivyo..na hapo ndipo wengi wanapaogopa..ila tusisahau wakati wewe unaogopa kukopa kuna wengine wanaendelea kutajirika kutokana na mikopo hii..Kwa kawaida mkopo una pande mbili..kuna upande wa kufukarisha na upande wa kutajirishwa,sasa inategemea wewe umesimama upande gani.

Hebu angalia upande huu nao:

Let's say umechukua mkopo wa sh 9,000,000/=
Umeingiza kwenye mzunguko wa biashara unaokuingizia angalau faida(net profit) 10,000/= kwa siku.Na hii ni biashara inayoingiza faida ndogo sana yaani <1%(0.11%)!

Kwa mwezi 10,000 x 30 = 300,000..kwa miaka mitano ni 300,000 x 60 = 18,000,000(faida tu)!
Kwa hiyo hadi miaka mitano inakamilika una jumla ya pesa: mkopo + faida: 9,000,000 + 18,000,000 = 27,000,000/=!
Sasa ukiwarudiashia benki 17,100,000 unabakiwa na (27m -17.1m) = 9.9m! Tuseme hiyo 0.9m inafidia gharama za kuprocess mkopo na mambo mengine ya hapa na pale.

Unaweza kuona kwamba ikiwa utakopa mkopo kwa ajili ya kujenga au kulipia ada,au hata kulipa deni,mkopo wa milioni 9 utatakiwa kulipa zaidi ya milioni 8 juu ya mkopo ule..ila kama utakopa na kuiweka kwenye mzunguko wa biashara,hadi unamaliza marejesho utabakiwa na milioni 9 mfukoni!
 
Mkuu umetema madini ya ukweli, ngoja nifikirie biashara itayoingiza net profit ya 10,000.
 
ametema ndio, aweke risk nazo

Mkuu kila kitu kina risk,lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba mkopo una maana ikiwa unauweka kwenye mzunguko wa biashara badala ya kukopa kwenda kulipa madeni na vitu kama hivyo..kikubwa mtu akope kuongezea au kupanua biashara ambayo tayari ipo na inarun vizuri.

Ni bahati mbaya kwamba wengi wetu,hasa wasomi,tunaweka mbele sana risks kabla ya uthubutu..ila tunachoweza kukubaliana ni kwamba dunia inaendeshwa kwa mikopo..matajiri wote unaowafahamu ni lazima ktk wakati fulani walijiendesha kwa kutegemea mikopo..
 
Umesema vyema na wanafanikiwa niwenye utayali wa kuthubutu...!
Point taken,
 
Hivi taasisi zote za kifedha hasa mabenk ukomo wao wa kukopesha ni miaka 5 tu hakuna wanaenda zaidi ya hapo?!
 
Yapo ila unaongezea na assets ili waweze kukuamini, ingawa haushauriwi kukopa kwa zaidi ya miaka mi5 hasa ukiwa beginners wa mikopo! Kimsingi miaka mi5 n mingi sana na ukiwa vzr unaweza kopa kwa miaka mi5 then ukiweka mambo yako sawa unalipa ndan ya miaka mi3-4,
 
Hivi NMB wana mkopo hadi miaka 5 kwa wafanyakazi?mbona mi niliambiwa kuwa wameanbiwa na mwajiri(serikali) mwisho ni miaka 3?
 
Back
Top Bottom