Kwa msiba mkubwa uliompata MC Pilipili na jinsi alivyopokea hakika nimejifunza mengi

Kwa msiba mkubwa uliompata MC Pilipili na jinsi alivyopokea hakika nimejifunza mengi

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Miaka kadhaa nyuma nikiwa naangalia mahojiano kati ya Mtangazaji na Mwanamuziki Mkongwe Mzee Zahiri Ally, kupitia ITV (kama sikosei maana ni muda sasa)...nakumbuka jibu la Mzee Zahir baada ya Mtangazaji kuonyesha wasiwasi wake kwa vipi Mzee Zahiri alimudu Jeshini kwa kuangalia muoenekano wake, ingawa sikumbuki moja kwa moja maneno ya Mzee Zahir ila nakumbuka alisema au alimaanisha "kwa nje naonekana laini lakini nina moyo wa simba"

Nimehitaji kusikiliza vyanzo zaidi ya kimoja kujiridhisha namna Mc Pilipili alivyopokea taarifa za habari ngumu kama ile na namna alivyoendelea kubaki imara kana kwamba kilichotokea si cha kumshtua sana, labda ni tofauti kabisa na wengi nikiwemo mimi ambavyo tungetarajia haswa kwa muonekano wa nje wa Ndugu yetu huyu.

Sidhani kama kuna mashaka yoyote juu ya nafasi, ukaribu au upendo wa Mtu kama Mc Pilipili kwa Mama yake yule.

Kuna wakati natamani kutupa lawama kwa namna ambavyo Muendesha Bajaji yule aliyekuwa amewabeba Majeruhi/Marehemu alivyopeleka taarifa ile 'kishamba' bila kujali kwamba angeweza kusababisha maafa mengine kwa wengine...lakini kwa upande mwingine ndiye aliyetupa picha halisi ya ndugu Pilipili.

Nadhani ni wengi tumeshashuhudia Watu Wakubwa wanaoonekana Wababe, Jasiri au Wasiogopa chochote kufikia kuangua kilio au kupoteza kabisa muelekeo, au kupatwa na mshtuko mkubwa kwa muda pindi wanapofikwa na taarifa za kushtua kuhusu Watu wao wa karibu.

Ndugu yetu huyu alipokea taarifa za tatizo lililowapata Wapendwa wake, tena ni Watu aliokuwa nao eneo hilo muda mfupi uliopita. Wengi labda tungetarajia Mtu hata kupoteza fahamu kama sio kuangua kilio kisichomithilika., lakini la hasha Bwana huyu aliendelea na shughuli aliyokuwa anaifanya mpaka mwisho...kwangu hii ni nguvu ya ajabu na ya kipekee sana.

Huyu bwana ni very strong, na amenifundisha kuwa siku zote "don't judge the book by its cover"

Nichukue nafasi hii kumpa pole Mc Pilipili na ndugu jamaa na Marafiki kwa Msiba wa Mama zake, Mungu amfanyie wepesi na Pumziko La Amani wapate Wendazao hao.
 
Huezi jua nje ya social media anaugua kiasi gani.
Mimi sijaona jinsi alivyopokea hizo habari za msiba bali maweza kusema yule bwana anaugulia kupita kiasi hata kwa maneno na clips zake ndogo ndogo.
 
Ni ujinga kupima ni namna gani mtu ameguswa na msiba kwa kumuangalia tu kwa nje au kwa maneno tu ya mdomoni....kwahiyo inabidi libakie tu kua ni swala la mtu binafisi na kuendelea kulijadili ni uendawazimu
Sijui kwako, ila kwangu kama alipewa taarifa na akaendelea na shughuli aliyokuwa anaifanya mpaka mwisho hiyo kwangu sio kawaida.

Unless kama unamaelezo tofauti na nilivyopata taarifa mimi ndio unijulishe.
 
Dunia imejaa mawazo hasi. Kuna wanaosema ni kafara kana kwamba alitakiwa kuishi milele. Mtuambie na Nyerere nani alimtoa kafara. Si alikuwa baba wa taifa?
 
Dunia imejaa mawazo hasi. Kuna wanaosema ni kafara kana kwamba alitakiwa kuishi milele. Mtuambie na Nyerere nani alimtoa kafara. Si alikuwa baba wa taifa?
Binadamu huwa hawakosi la kusema kwa chochote kinachotokea.
 
Binadamu huwa hawakosi la kusema kwa chochote kinachotokea.
Ila sio vizuri kumsema vibaya mtu aliyeondokewa na mzazi maana maumivu yake ni makubwa. Kila mmoja atashuka kaburini iwe kwa kuugua au kuuawa. Tusiwe wepesi wa kumnyoishea mtu kidole linapotokea jambo kam hili.

Darlin
 
Sijui kwako, ila kwangu kama alipewa taarifa na akaendelea na shughuli aliyokuwa anaifanya mpaka mwisho hiyo kwangu sio kawaida.

Unless kama unamaelezo tofauti na nilivyopata taarifa mimi ndio unijulishe.
Moyo wa Simba.
 
Moyo wa Simba.
Anafaa kuwa Kiongozi wa Jeshi maana Mwanajeshi hawezi kuangua kilio au kuonyesha unyong'onyevu mbele ya Askari anaowaongoza hata kama ameambiwa jambo gumu kiasi gani.
 
Kwani pilipili ndiye wa kwanza kufiwa na mzazi hadi ajadiliwe humu?
 
Kwani pilipili ndiye wa kwanza kufiwa na mzazi hadi ajadiliwe humu?
Kinachojadiliwa hapa ni namna alivyopokea taarifa ya msiba wa ghafla wa Mama yake na Mama mdogo na namna alivyoweza kuendelea na shughuli aliyokuwa anaifanya kwa wakati huo mpaka walipomaliza ndio wakaanza na suala la msiba.
 
Back
Top Bottom