Miaka kadhaa nyuma nikiwa naangalia mahojiano kati ya Mtangazaji na Mwanamuziki Mkongwe Mzee Zahiri Ally, kupitia ITV (kama sikosei maana ni muda sasa)...nakumbuka jibu la Mzee Zahir baada ya Mtangazaji kuonyesha wasiwasi wake kwa vipi Mzee Zahiri alimudu Jeshini kwa kuangalia muoenekano wake, ingawa sikumbuki moja kwa moja maneno ya Mzee Zahir ila nakumbuka alisema au alimaanisha "kwa nje naonekana laini lakini nina moyo wa simba"
Nimehitaji kusikiliza vyanzo zaidi ya kimoja kujiridhisha namna Mc Pilipili alivyopokea taarifa za habari ngumu kama ile na namna alivyoendelea kubaki imara kana kwamba kilichotokea si cha kumshtua sana, labda ni tofauti kabisa na wengi nikiwemo mimi ambavyo tungetarajia haswa kwa muonekano wa nje wa Ndugu yetu huyu.
Sidhani kama kuna mashaka yoyote juu ya nafasi, ukaribu au upendo wa Mtu kama Mc Pilipili kwa Mama yake yule.
Kuna wakati natamani kutupa lawama kwa namna ambavyo Muendesha Bajaji yule aliyekuwa amewabeba Majeruhi/Marehemu alivyopeleka taarifa ile 'kishamba' bila kujali kwamba angeweza kusababisha maafa mengine kwa wengine...lakini kwa upande mwingine ndiye aliyetupa picha halisi ya ndugu Pilipili.
Nadhani ni wengi tumeshashuhudia Watu Wakubwa wanaoonekana Wababe, Jasiri au Wasiogopa chochote kufikia kuangua kilio au kupoteza kabisa muelekeo, au kupatwa na mshtuko mkubwa kwa muda pindi wanapofikwa na taarifa za kushtua kuhusu Watu wao wa karibu.
Ndugu yetu huyu alipokea taarifa za tatizo lililowapata Wapendwa wake, tena ni Watu aliokuwa nao eneo hilo muda mfupi uliopita. Wengi labda tungetarajia Mtu hata kupoteza fahamu kama sio kuangua kilio kisichomithilika., lakini la hasha Bwana huyu aliendelea na shughuli aliyokuwa anaifanya mpaka mwisho...kwangu hii ni nguvu ya ajabu na ya kipekee sana.
Huyu bwana ni very strong, na amenifundisha kuwa siku zote "don't judge the book by its cover"
Nichukue nafasi hii kumpa pole Mc Pilipili na ndugu jamaa na Marafiki kwa Msiba wa Mama zake, Mungu amfanyie wepesi na Pumziko La Amani wapate Wendazao hao.