Kwa mtaji wa 25 million nifanye biashara gani?

Mandison

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
191
Reaction score
110
Sijawahi kufanya biashara ya aina yeyote isipokuwa nimefanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 25/- milioni ambazo nafikiria kujiajiri kwa kufanya biashara.

Naomba wazoefu wa Jiji la Dar mnipe ushauri juu ya biashara ya kufanya tafadhali.

Maoni ya wadau:
Biashara za mazao zinalipa sana, na kwa mtaji huo naamin unatosha kabisa kuanza biashara hiyo lakini biashara zipo nyingi, cha msingi angalia wewe unapenda nini maana itakuwa rahisi kukifanya na kukisimamia ili upate faida zaidi
Mimi nashauri ufanye biashara ya kuimport vyakula jumla jumla hapo kama unatoa Mbeya viazi unaleta mjini au ndizi Bukoba unaleta mjini ni biashara nzuri ukipata dalali mwenye wateja wengi
Chukua mil.5 tafuta sehemu yenye muonekano mzuri na watu wengi fungua COSMETICS and mambo ya kutengeneza kucha wadada.
 
Nunua bajaji 3 za kuanzia hela nyingine iwe ya emergency waambie kila siku wakupe elfu kumi tu kwa mwezi utakuwa na laki 9 biashara safi angalizo bajaji zisifanye kazi zaidi ya saa kumi na mbili jioni zinaibiwa sana
 
Mtaji mkubwa sana huo na vilevile mtaji mdogo sana huo.
Cha msingi usiiweke ela yote kwenye kitu kimoja, igawanye hata mara 3.

Ili biashara yeyote iwe na mafanikio endelevu ni lazima kuangalia usalama wa mtaji kwanza kabla ya kuangalia faida.
Ni sawa, ila ni biashara gani sasa?
 
Kuna uwezekano mkubwa sana wa wewe kuzipoteza hizo hela kama utafata ushauri wa watu humu jukwaani
 
kuna uwezekano mkubwa sana wa wewe kuzipoteza hizo hela kama utafata ushauri wa watu humu jukwaani
Inategemea ni ushauri gani na pia wanasema akili za kuambiwa changanya na zako..
Baada ya hapo hutomlaumu aliyekupa ushauri kwani ulipata nafasi ya kuchuja huo ushauri na kuona faida na hasara zake.
Tusiwakatishe tamaa wale wenye moyo wa kujitolea kuwapa wenzao ushauri humu jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…