Kama utaona yakufaa fanya hivi:
1. Nunua pikipiki 5 jumla ni milioni 10. Wape vijana kwa mkataba wa kisheria wakupe elfu 10 kwa siku baada ya Mwaka unamwachia pikipiki. ( uwape mkataba wa kisheria akipoteza anakulipa) kwa siku ni 50000 sasa itakuwa 50000×365 = 18,250,000
Faida kwa mwaka ni 8,250,000. Kwa mwezi ni kama 687,500.
2. Fungua M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money & Halopesa mahali vibanda viwili pia usajili laini hapo hapo. Kibanda cha kwanza mtaji 2mil, makadirio ya commission 350,000 (mfanyakazi laki, kibanda 50,000, umebaki na 200,000)
Kwa hiyo vibanda viwili baada ya kodi na mishahara yao makadirio ya faida ni 200,000 × 2 = 400,000 Fanya 350,000 incase of anything.
Milioni 6 Iliyobaki: 3mil weka M-Pawa au fixed account ikulinde.
Milioni 3 nyingine fungua kaduka fulani kadogo lakini ka wadhifa weka vyakula au bidhaa za urembo (au yoyote isiyooza) Soma soko lakini 'ANZIA SOKONI' Hapo utapata hela ya kula daily, vocha, home kuacha elfu 5 kama una familia.
Kwa haraka haraka utakuwa umetengeneza mshahara 687,500 (pikipiki) + 350,000 (M-Pesa n.k) = 10337500 yaani milioni kila mwezi.
Kumbuka mtaji wako uko pale pale ndugu. Kila la heri na shetani asipite huko maana kazidi.