Kwa mtaji wa 50 Milioni nizalishe bidhaa gani niingize sokoni kuutafuta utajiri

Kwa mtaji wa 50 Milioni nizalishe bidhaa gani niingize sokoni kuutafuta utajiri

Wakuu habar zenu nafikiria kufungua kiwanda yaan kununua machine kwa ajili ya uzalishaji

Sasa kwa mtaji wa Milioni 50 naweza kununua machine za kuzalisha bidhaa zipi ambazo nitaweza kuingia sokoni kuusaka utajri maana nimeiona biashara za uchuuzi zitanichelewesha sana

Wadau leteni mawazo yenu
Unajua mpaka leo hii, Tanzania tunagiza toothpick nje ya nchi? Stick za kuchomea nyama(mishkaki) pia hatutengenezi! Malighafi zipo(mianzi) ipo kibao iringa na Morogoro hapo.
Mashine complete(production line) niliuliza haizidi 15M pesa ya kitanzania pamoja na kodi.
Hebu jaribu kulichakata hili wazo la biashara, alafu tafuta mshauri.
 
Fikiria product ambayo haitakuwa na ushindani na utitiri wa bidhaa za mchina zilizojaa sokoni. Kumbuka wale cost of production kwao iko chini sana.
Kama ni lazima uwe na mashine basi ziwe za food processing.
 
Unataka utajiri ama kufanikiwa?.

Kama unataka kufanikiwa piga shughuli zote legally kitaani zinazotambulika na serikali pia zingatia location, connection, good advisers, mfano shughuli za madini, kilimo na biashara.

Ila kama unataka utajiri, wewe nenda kwenye the most riskier activities ambazo kama ukipata ujuwe umepata, na kama utapoteza ujuwe utapoteza kweli kweli, the more you risk the more you will double your capital.

Hapa nazungumzia activities kama Forex , Cryptocurrency, betting, gambling n.k

Kwenye Crypto hasa kwa msimu huu kila Coin inadump/going down baada ya big Camps/investors kuondoa/sell holdings zao, hivyo wanaacha big DIP ya new buyers kutake place early before pumping season haijaanza.

For now let's say Bitcoin, Ethereum, solana, BnB zinapitia downtrending ya hatari ambapo indicators zinaonesha baadhi ya hizi Coin zimefikia strong Support level/ lower level of all time low ukilinganisha na last December, then after hii season ya Hollidays za Christmas na new year kuna uwezekano wa incoming High volume itakayopump mamia ya Coins/tokens 2x, 5x, 10x- 100x, suala la muda tu, ktk cryptocurrency hakunaga kupoteza kabisa bali kuna kuchelewa kuondoa Loss of capital.

Chukua $20,000(Milion 49) tia kwenye Solana, BTC, XRP, Doge, BnB na baadhi ya altcoins/token ambazo zita adopt volume gaining, $20,000+possible 10x kutoka ktk ''10''assets kila moja ukapata 100% of profit = $20,000+1000% = $220,000 = 548,900,123 Tsh of total profit.

then rudia the right process for the next 10x possibility baada ya ku-Cut off short losses within 3 months unazaidi ya bilion za kitanzania.

Njia ya pili hapa hapa kwenye cryptocurrency, take $20,000 nunua 10 Memecoins kutokea BnB network/solana network each token kwa $2000 at early market cap, take profit target ni 1000%, then $2000*1000%×5*2= $200,000 = 499,000,111 Tsh (milion 499), rudia hii process Kwa next trading kwa chance ya 10x-100x.

WHAT A GOAL? malengo ushatimiza, do your own research, hii sio recommendation wala ushauri wa kuuzingatia bali maoni tu uyafuate au yapotezee.

Nalog Off..

Note: haya ni maoni yangu tu asitokee mpumbavu mmoja mjuaji wa kuleta ujuaji wake hapa
 
Kiwanda hakikupi utajiri wa chap chap hivyo maana una kazi ya kutengeneza wateja wako kwanza

Ila uzuri wa kiwanda ni uwezo wa kutengeneza generation wealth na ni biashara ambayo ni scalable

Utajiri wa chap chap ni uchuuzi nenda china kafyatue copy leta bongo
 
Fanya biashara ya kununua na kuuza viwanja kwa ajili ya makazi ya watu, hasa hasa maeneo ambayo miji inaanza kukua
 
Tafuta eneo 10m.
Funga poultry cages 5, 30metres 15m
Chini yake chimba vertical fish reservoirs kwenye kila cage 15m

5m tafuta kuku, fuga and chini 2m weka samaki (mbegu), zile wastes kutoka kwenye cages za kuku zitakuwa chakula cha samaki.

3m endeshea.

Possible income kwa siku 60 ni 20m
 
Wakuu habar zenu nafikiria kufungua kiwanda yaan kununua machine kwa ajili ya uzalishaji

Sasa kwa mtaji wa Milioni 50 naweza kununua machine za kuzalisha bidhaa zipi ambazo nitaweza kuingia sokoni kuusaka utajri maana nimeiona biashara za uchuuzi zitanichelewesha sana

Wadau leteni mawazo yenu
Knowledge vs experience

Invest hiyo hela kwenye experience uliyonayo sio knowledge uliyonayo

Una experience gani kichwani kwako katika jambo lolote lile ambayo unaijua in and out
 
Unajua mpaka leo hii, Tanzania tunagiza toothpick nje ya nchi? Stick za kuchomea nyama(mishkaki) pia hatutengenezi! Malighafi zipo(mianzi) ipo kibao iringa na Morogoro hapo.
Mashine complete(production line) niliuliza haizidi 15M pesa ya kitanzania pamoja na kodi.
Hebu jaribu kulichakata hili wazo la biashara, alafu tafuta mshauri.

Mm nilikuwa nina wazo kama hili.
 
Back
Top Bottom