Part 3:
Project ya vitunguu ; hii inaweza kukutoa kabisa kwenye umasikini ila inahitaji kujifunza na kufika eneo sahihi. Kwa mtu unaejitafuta unatakiwa uwe makini sana na ufuatilie data zinavyobadirika. Soma trend ndani ya mwaka price viriation inavyokwenda.
"Boom and recession" zinatokea wakati gani. Kutoka hii july mpaka sept unaweza pata vision ya bei ya jan to may 2025 ambapo itakuwa aidha Booom au recession.
Mwaka huu niliiona trend ila kwa sababu sikuwa mazingira rafiki sikulima ila pesa niliziona kabisa kwa trend ilivyoenda.
Sasa unatakiwa ujipe task ya kufuatolia uzalishaji wa kutunguuu ulivyo sasa na bei iliopo kisha weka mkakati. Price kwa sasa sio mbaya hasa huku Njombe na Mbeya vinapolimwa vitunguu.
Ubaya wa vitunguu vikiporomoka vinakuwa lita sh 500 hapo lazima ikukate.
Kwa hio mil3 zako zinaweza kukupa milioni 10 ndani ya miezi 3. Vitunguu unalazimika ufuate mabonde ya vitunguu TZ. Sio kila mahala vinastawi vitunguu bali baadhi ya maeneo tu.
Maeneo mazuri ni Singida, Mbeya, Njombe, Arusha na Morogoro. Huko ndio maarufu na wanamisimu tofauti, sina hakika kama kwetu kigoma kuna bonde linalostawisha vitunguu vya KIBIASHARA.
Mimi binafsi kama trend itaenda vizuti ningekushauri ulime vitunguu msimu ndio huuu na utavuna na kwenda kulima tena maharage kama part 1 na 2.
Maharage ni zao lenye kipato kisichokuwa kikubwa na yakupasa ulime pakubwa sana il8 utoboe kimahesabu. Vitunguu heka moja unaweza pata faida mara 5 ya maharage kwa mtaji ule ule.
Vitunguu vinahitaji skillls kubwa sana kuvilima kulinganisha na maharage. Vitunguu zaidi ni kiangazi na maharage ni mda wote. Kama utachagua kulima vitunguu safiri uende kwenye mabonde ya vitunguu.
Usilime mazao ya mazoea kama mpunga au mahindi. Trend yake huwa haisomeki. Boom nzuri ipo kwenye vitunguu, Viazi mviringo na nyanya za masika. Naishia hapo.
Linda mtaji wako usikurupuke utafilisika, chagua eneo litakalokupa matokeo ya haraka.