3m ni nyingi sana,kuna mazao ya mboga mboga ukipata eneo lenye maji,kwa maana kilimo cha umwagiliaji,mazao ya mboga yasio na usumbufu Bamia na Ngogwe yanaweza badili kabisa maisha...
Binafsi nimegundua wa TZ wengi kuna ka sehemu hua tunajizima data kidogo,mfano...tuseme mtu ana shamba lake mahali ekari 10 halina rutuba ama maeneo hayo mvua sio nzuri na kwa ujumla mazao hayatoki,ila tunakomaa hapo hapo miaka na miaka,hili ni kosa kubwa kwa muono wangu,ni bora ukakodi hata ekari 5 sehemu nzuri na yenye uhakika wa kupata mavuno bora ukakimbiza.
Turudi kwenye mboga mboga,
1.Bamia
Unaweza kodi shamba ekari 2 kwa laki ama laki 2 kila ekari,ukafanya ya kufanya ukapanda na ukazisimamia vizuri,mbegu za bamia ni 15,000/Kg na ekari moja utapanda kilo 3-4,zinakua haraka,hazina purukushani ya mbolea,changamoto za wadudu na magonjwa ni za kawaida,utavuna miezi 3 na utachuma kila baada ya siku 2 kwa muda huo wote,mchumo wa chini wa ekari haupungui debe 10 na mchumo wa juu debe 30 kwa mbegu hizi za kienyeji,ukitumia hybrid itazaa zaidi na muda mrefu zaidi,
Debe haliwezi pungua Tsh 3000 hata iweje,kuchuma 500 kwa ndoo ya kutolea shambani,ama 700 kwa kipimo cha ndoo ya kuuzia,na kiwango cha juu kinaweza fikia 15,000 kwa debe wakati gharama zingine zote ni zile zile.
Unaweza piga hesabu unaweza ingiza kiasi gani kipindi hata cha kiangazi,
Na hapa ndipo pa kutengeneza mtaji wa kulima kilimo kikubwa cha mazao mengine wakati hii ina ku sustain,hutoi hela mfukoni.
Kumbuka,eka 2 ya bamia kwa 700,000 inaweza kukulimia ekari 20-50 ya mahindi/maharage/ufuta/mbaazi/ekari 10 ya karanga na mazao mengine yanayo ota vizuri na yenye soko yatakayo kupendeza.
Kwanini nimekushauri Bamia?
Sio labour intensive,soko lake ni uhakika,na ni kilimo cha bei nafuu,eneo dogo litakupa faida kubwa,eneo dogo ni rahisi kuli manage(mfano kupiga dawa unakomaa mwenyewe-ila zingatia maziwa pembeni ukimaliza unakunywa) etc
2.Ngogwe...,hapa ni waache kwanza mmeze hiyo ya Bamia