Kwa mtaji wa milioni 3 naweza kuingia shambani nikalima kisasa?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Huu ulimwengu, game ni tight sana hasa upande wa kutafuta pesa, kuna saving zangu kama million 3 nimeamua kurisk shambani sina matarajio makubwa lakini najua itakua ni sehemu ya kujifunza.

Hii mada inahusu wazoefu tu, nipo kasulu nafikiria kulima maharage na mahindi kwa msimu unaokuja, nimejaribu kutafuta bonde lakini mambo yamekua magumu, watu wanalima kwa kutegemea msimu, kuna watu waliojaribu kulima mbali na wanapoishi?

Yaani mfano nakaa kasuku alafu nalima singida? /Mbeya?
 
Hela inatosha sana hiyo Kwa mkoa ulioutaja ila Lima heka mbili za maharage, mahindi Lima heka Moja Kwa haraka ukilima Kwa msimu matumizi yote ayawezi zaidi 1.3 m na inabidi upige kambi uko uko kilimo Cha Simu kimewagalagaza wengi.
 
Labda kienyeji
 
Shukurani hii nimeichukua, na sehemu gani unapendelea zaidi? Uvinza, kasulu? Au kibondo? Nipo kigoma mjini
 
Asante sana
 
Hii sehemu sijaelewa, "mbolwa ya kuku gunia tano ni nini? Au unamaanisha mbolea ya kuku gunia tano?, then nilikuuliza unanishauri kilimo changu nifanye wilaya hipi? Au popote yanakubali? Kesho nilikua na tour ya kwenda kasulu nikafatilie mashamba.
 
Samahan, huyo mtusi naeza pata namba yake mapema kabla sijaanza kilimo?
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…