Kwa mtaji wa Tsh. 400,000/- naweza fanya biashara gani?

Wazo zuri... Kuna kijana amefanya kitu kama hiki pale mtaani kwetu, kafungua ana miezi miwili sasa. Anasababisha karibia kila siku nakula kuku[emoji39], na wateja wanaongezeka kila siku ila yeye kuku anachoma.
Anaanza kuuza mida ya saa 9/10
 
Wazo zuri... Kuna kijana amefanya kitu kama hiki pale mtaani kwetu, kafungua ana miezi miwili sasa. Anasababisha karibia kila siku nakula kuku😋, na wateja wanaongezeka kila siku ila yeye kuku anachoma.
Anaanza kuuza mida ya saa 9/10
anachoma na mafuta au na mkaa? Maana kiswahili hiki kigumu kidogo,wapo wanaochukua nyama wakachoma kama maindi mfano wa kubanika kuna siku nilionja nikashangaa utamu wake 😜😝
 
Duh..!!,huyo kuku wa 18,000 Ni kuku au ndege mwarabu mkuu?,maana hiyo Bei inakaribia Bei ya mwanambuzi
Ndio maana kila kitu hapo nimeandika Makadilio nina maana si bei halisi inaeza kupungua au kuongezeka,. em nawewe toa ushauli wako wadau wapate faida.
 
Fungua duka mkuu. Mobile shop. Unanua vtu unatembeza majumbani, hakikisha umestidy demand kwanza....and spending pattern


Sent using Kirikuu
 
Hicho Kisiwa kipo ndani ya wilaya/mkoa gani? Na Logistic za kufika hapo zikoje?
 
anachoma na mafuta au na mkaa? Maana kiswahili hiki kigumu kidogo,wapo wanaochukua nyama wakachoma kama maindi mfano wa kubanika kuna siku nilionja nikashangaa utamu wake 😜😝
Hahahaa anachoma kama mahindi, yeah ni watamu mno ukikuta anayejua kumarinate vizuri.
Me napenda sababu nyama inakua haina mafuta mengi tofauti na wale wa kukaanga
 
Hahahaa anachoma kama mahindi, yeah ni watamu mno ukikuta anayejua kumarinate vizuri.
Me napenda sababu nyama inakua haina mafuta mengi tofauti na wale wa kukaanga
Unanijaza mate mdomoni nakumbuka ni kweli wanaradha flani ivi yatofauti
 
Wakuu! Mm Nataka kufanya biashara ya nazi,

Nazi Nataka kuzitoa Lindi, na kuuzia dsm

Mwenye informations zaid naomba anijizu, hasa kuhusu masoko ya dsm kwa upande wa nazi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Uzuri wa biashara, jitoe akili kabisa

Usiweke analysis nyingi

Fanya kama akili imefyatuka, hapo utatoboa

Kupoteza pesa yote bila return ni kitu cha kawaida.

Kuna faida na hasara pia, so unakuwa tayari kwa lolote

Never give up, ni kuamka na kupambana
 
Ni kweli kabsa mkuu tena biashara zenye risk kubwa ndo zinatoa faida kubwa kama zikiti vzr
 
Faida ni kubwa kuliko hasara,
Mfano:
Mahindi kilo 1 yanaweza toa bisi zenye thamani ya 6000/= to 7,000/= au zaidi,
Kwasiku waweza bangua zaidi ya kilo 1.
Mahindi= waweza nunua 1,300 hadi 1,500 kwakilo kutegemea eneo uliopo,
Mafuta ya 1,000/= utosha kabisa kwa kilo nakubaki kidgo.
Hapo waweza ongeza sukari kidogo au chumvi n.k kuleta utam zaidi ambapo thamani yake ni ndogo tu.
Pia, kuna watu watafika langua kwako au kubangurisha mahindi yabis kwako, waweza pata order kwenye hizi sherehe...
Umeme hutumika kidogo sana, (kuna zitumiazo gesi pia),
Haina haja yakutafuta frame waweza anzia hata nje yaduka/frame yamtu, ukiamua hata kwako nakuwapa vijana wazungushe

Hasara zimemezwa nafaida, changamoto kubwa ni kupata eneo zuri (wateja wapo watoto kwawakubwa) hapo ni wewe tu kuongeza ubora.

Gharama yauendeshaji ni nafuu sana,(pango +mahtaji)




samahani mkuu hiyo biashara ya bisi ikoje unaweza fafanua kdg.faida na hasara zake piah



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaa anachoma kama mahindi, yeah ni watamu mno ukikuta anayejua kumarinate vizuri.
Me napenda sababu nyama inakua haina mafuta mengi tofauti na wale wa kukaanga
Alafu ngumu kumanage ishu ya mafuta, unakuta mtu anatumia mafuta mda mrefu mpaka yanabadilika rangi yanakuwa meusiiiiii, bora wa kuchoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…