Kwa mtaji wa Tsh. 400,000/- naweza fanya biashara gani?

Ewaah! Hapo jinsi ya kutengeneza
 
Ewaah! Hapo jinsi ya kutengeneza
Wanatengeneza hivo mkuu....ukiongeza kamba za katani kwa juu kwa package kubwa inakuwa nzuri....kwa ndogo acha hvohvo tu.....hakikisha zinakuwa na ukubwa mbalimbali nyingi ziwe na ule ukubwa wa rambo za 100 zamani....

Ukishindwa elewa hizo picha, jaribu kugoogle how to create paper bag youtube au kwa kiswhaili jinsi ya kutengeneza mifuko ya kaki/vifungashio vya kakiView attachment 1726604
 
Umeongea point kubwa Sana mkuu
 
Mkuu kwenye bahasha za kaki hapa msaada kidogo
Je vile vibasha vidogo unauza kwa jumla vikiwa vingapi na bei unachaji vipi?
Na zile kubwa bei zipoje ?
 
Mkuu kwenye bahasha za kaki hapa msaada kidogo
Je vile vibasha vidogo unauza kwa jumla vikiwa vingapi na bei unachaji vipi?
Na zile kubwa bei zipoje ?
mkuu zile kwa ninae mjua anauza jumla kubwa kiasi ni 300 na ndogo ni 200 jumla.....sijajua kwa maeneo mengine maana kila mtu anabei yake ila cha kukumbuka ni kuwa bahasha kubwa inauzwa 400 dukani wewe inabidi uuze bei ya chini yake ndio maana anauza 300.....na ofcourse huwa maduka ya mjini wanamuungisha hadi bahasha 40 kwa siku.hizo kubwa huwa anamake 12000 ukitoa hela ya kununulia karatasi na gundi hakosi elfu 8 hadi elfu 9.

Ila kama kwenu bahasha kubwa zile zinauzwa 500 hadi 600 wewe uza zako 400 kwa jumla reja 300.
 
Nashukuru ngoja nifanye kautafiti huku mtaan kwetu .
 
Nina mtaji wa sh laki nne je naweza fanya biashara gani kama ujasiriamali?
1.Kijiwe cha kahawa.
Wazo langu laweza kuonekana la kipumbavu ila fungua kijiwe cha kahawa na kashata mkuu. Tafta eneo la stand au sokoni. Utajipatia chochote kitu daily. Kashata inatoa faida nusu kwa nusu. Unaweza kuwa mbunifu ukatengeneza kashata ambayo badala ya kuiuza sh.100 we utaiuza sh.500 itie hata flavour ya maziwa tu.

Vikombe vikubwa vya kahawa hata ukiuza kimoja jero sio mbaya. Mwanzo utakuwa mgumu ila wakikuzoea utakuwa umejenga base ya wateja wako maalumu. You will make money indeed. Pia weka na uji kama itafaa.

2.Kijiko cha nyamachoma.
Hii utanunua nyama za mafungu vingunguti pale. Utaanza kuzibanika mida ya jioni location iwe stand au kwenye barabara za makutano karibu na kituo cha daladala. Kata bei ya buku buku kwa kipande then unavibanika na kuwawekea na pilipili na ndimu pembeni au vinegar. Utatumia foil ku serve hio nyama ili usipate gharama ya kuosha osha sahani. Hakikisha usafi wako binafsi na mazingira ya meza unayofanyia kazi ambayo pembeni ndio itakuwa na jiko.

3.Kijiwe cha pweza.
Hii pia ni biashara nzuri ukiwa location nzuri. Utakula vichwa kama uko maeneo ya kituo cha daladala pembeni. Huwa lazma nitafunege wale wadudu mara nyingi na huwa sio ghali sana. Hii inaashiria hata mtaji wake hautakuwa mkubwa pia.

Mkuu jaribu hizo..Mtaji wake hautafika hata nusu ya hio hela ili ubakiwe na chenchi ya kusapoti biashara kadri inavyoanza kukua taratibu maana biashara inataka uvumilivu sana.
 
Biashara ni betting ambayo inakuwa real life na wewe ndio Key Player 😂
 
Mkuu uliacha biashara inayolipa ukaenda kuwa mtumwa?
 
Ukisema bahasha kubwa unamaanisha size ipi kubwa kuliko A4 =A4, mifuko mbadala shingapi

Ndugu yang anauza lakini si ya kaki some local ukilinganisha kwa makaratasi hadi makighafi na hiyo Size ya A4 anauza mifuko 30 kwa 1000 hizi bei ulizoandika wewe naona zinameremeta.
 
Mawazo mazuri mkuu. Humu jf ukitulia lazima ufanikiwe.
 
Mkuu uliacha biashara inayolipa ukaenda kuwa mtumwa?
Mkuu nilikosa eneo maana nilikuwa naifanya kimachinga naotea mtu asipokuja ndio nacover sehemu yake, leo nipo huku kesho kule nikaona nirudi kuwa mtumwa....

Ika nitaifanya najipanga sana mshahara asilimia 80 wote nauweka akiba mwezi wa 12 nianzishe biashara 2 mkuu ndogo ndogo
 
atengeneze kwa kaki mkuu, na auze jumla kwa bei hiyo haswa maduka ya mjini ya nyama, nguo, maduka ya mahitaji ya nyumbani etc atapata hiyo faida maana namimi nimenunua mara kadhaa kwa jamaa nikiwa mjini kwa bei ya 300 moja.
 
Ndiyo mkuu ni size ya A4 mkuu maana ndio size bora ya vifungashio
 
kwanini usianza ukiwa chuoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…