#COVID19 Kwa mtazamo wangu Covid-19 haipo Tanzania, tusitishane

#COVID19 Kwa mtazamo wangu Covid-19 haipo Tanzania, tusitishane

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mimi binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Tanzania tuna corona.

Nchi hii bwana watu wanaotutangazia kwamba tuchukue tahadhari ndio haohao unawakuta baa wanakunywa pombe na kukumbatia mpaka wahudumu.

Unawakuta anayetutangazia corona yeye ndiye wa kwanza kwenda msikitini au kanisani kubanana wakati wa kusali.

Leo unasema Dar kuna corona wakati pantoni ya kwenda Kigamboni inapakia watu mpaka elf 1000 kwa mkupuo na watu unakuta wameshonana kwenye jengo la abilia ni full kutoka jasho.

Unakuta mtu tena very smart eti yupo kwenye mwendokasi amevaa barakoa huku kasimama anasweti tu yaani kabanwa mpaka sehemu ya kupumulia hana halafu kapiga barakoa yake nayo inatoa tu jasho.

Mimi kanisani ninakosali tunabanana balaa muda wa kutoa sadaka tunagusana balaa na muda kuondoka tunabanana kwenye usafiri kwa kupeana lifiti.

Kiufupi wanaotangaza uwepo wa corona Mimi nawashangaa sana kwanini hawaji na taratibu za mapambano ya dhati?

Hivi unapambana na corona kwa style ya kariakoo ile? Na daladala za Mbagala?

Serikali waache siasa labda kama corona ya wanayoisema inawahusu wao viongozi sawa huku mtaani Mimi sioni corona tena baada ya Kifo cha Magufuli.
 
Wanafosi ionekane ipo ili nchi ipewe mikopo, Ukishupaza shingo hupewi mikopo.
 
Aisee nyinyi watu wa ajabu sana. Sasa nani anafaidika kusema Corona ipo wakati haipo, mimi nakushauri tembelea hospitali zote uliza kama wana wagomjwa wa corona au la ndio uje uandike uzi.
 
Unajifungia siku nzima chumbani kwako huko Buza unaangalia Series kwenye t.v bila kutoka nje, utajua vipi kuhusu Corona.

Nenda Muhimbili ukaone wodi zilivyojaa wagonjwa wenye tatizo la kupumua, na ujionee kwa siku moja wanapokelewa wagonjwa wangapi wenye tatizo hilo. Halafu ndio urudi kuendelea na hii mada yako.
 
Mkuu,

Kipindi Hayati Magufuli anasema Tanzania hakuna Corona si nyinyi humu jukwaani na wenzio kina Mshana, Erythrocyte na nyumbu wengne mlikuwa mnakesha kusema maiti zimezagaa mtaani kwa kufa kutokana na Corona, kwamba Jpm ni wauaji watu wanakufa halafu hawatangazi.

Sasa leo kimekusibu nn kuwageuka wenzio ndugu yetu?
 
Mkuu ni kweli 3rd wave imekuja maana serikali haipati faida yoyote kusema kuna Covid 19!! Zaidi itajiharibia tu kukosa watalii and the likes.

Lakini waTanzania hamuelewi mnataka nini. Magufuli alipopinga hakuna Covid 19 ilihali watu waliugua tukamsema humu, Mama Samia anajaribu kuwa muwazi tunaanza mkejeli.

Barakoa ni kama condom tu kwa VVU/STIs, haikulindi lakini ina control tu kuambukizana hasa kwa njia ya hewa. Sasa kwa kuwa kuna watu wanavaa condom vibaya n.k ndio ziachwe kabisa? Je Tanzania bila condom unadhani VVU ingekua imekula wangapi kuliko sasa??

Anyway kma unapinga watu kupanda pantoni wakiwa wengi ina maana unataka lockdown ili sasa msisongamane..... Yakitokea hayo tena mtakuja humu JF kumtukana mama.

Mie licha ya kutowahi mpenda JPM lakini nimeona alikua sahihi tu na udikteta wake maana Mama anajaribu kuwa lenient ila watu bado malalamiko mengi mnoo kila anachofanya.

Weird
 
Unajifungia siku nzima chumbani kwako huko Buza unaangalia Series kwenye t.v bila kutoka nje, utajua vipi kuhusu Corona.

Nenda Muhimbili ukaone wodi zilivyojaa wagonjwa wenye tatizo la kupumua, na ujionee kwa siku moja wanapokelewa wagonjwa wangapi wenye tatizo hilo. Halafu ndio urudi kuendelea na hii mada yako.
Weka picha hapa tuone!

Hivi mnafikiri huko muhimbili mnafika peke yenu?
 
Nyie makamanda uchwara mkiambiwa hakuna corona mnapinga na kusema ipo hadi bungeni mnajitoa; haya, sasa mnaambiwa ipo napo mnapinga, mnataka nini haswa?
 
Mkuu,

Kipindi Hayati Magufuli anasema Tanzania hakuna Corona si nyinyi humu jukwaani na wenzio kina Mshana, Erythrocyte na nyumbu wengne mlikuwa mnakesha kusema maiti zimezagaa mtaani kwa kufa kutokana na Corona, kwamba Jpm ni wauaji watu wanakufa halafu hawatangazi,,

Sasa leo kimekusibu nn kuwageuka wenzio ndugu yetu?
Nyumbu hawajawahi kuwa na akili
 
Hata mie nimeshangaa! Huu unafiki wa waTanzania
 
Weka picha hapa tuone!

Hivi mnafikiri huko muhimbili mnafika peke yenu?
We jamaa ndio usiongee, mtu mwenyewe unaishi Vigwaza ndani ndani huko hata umeme haujafika. Sim mnaenda kuchaji kwenye solar ya mwenyekiti wa kijiji.

Saa ngapi utajua mambo yanaoendelea mjini. Tuliza kizibo hicho kijana utuache wa mjini tuongee mambo ya kifamilia hapa.
 
Mkuu kuna pesa ya corona, juzi uganda walikamatwa wanazika majeneza matupu
 
We jamaa ndio usiongee, mtu mwenyewe unaishi Vigwaza ndani ndani huko hata umeme haujafika. Sim mnaenda kuchaji kwenye solar ya mwenyekiti wa kijiji.

Saa ngapi utajua mambo yanaoendelea mjini. Tuliza kizibo kijana utuache wa mjini tuongee mambo ya kifamilia hapa.
Kwa coment yako hii tu tayari umeshajionyesha wewe ni mtu wa aina gani!

Jf imebeba kila takataka ni kuvumilia tu
 
Unajifungia siku nzima chumbani kwako huko Buza unaangalia Series kwenye t.v bila kutoka nje, utajua vipi kuhusu Corona.

Nenda Muhimbili ukaone wodi zilivyojaa wagonjwa wenye tatizo la kupumua, na ujionee kwa siku moja wanapokelewa wagonjwa wangapi wenye tatizo hilo. Halafu ndio urudi kuendelea na hii mada yako.
Toka mwezi uliopita alikua mgonjwa mmoja tu ambae alishapona mda mrefu, mpaka jana jioni sjaona mgonjwa mpya wa corona muhimbili
 
Sijui umekuwaJe leo technically ?! . Hospital kubwa kama BMC imepoteza madaktari wake kwa hii kitu . Wewe Leo unaleta siasa za Jiwe ?!. Jiwe mwenyewe imemuonyesha kilichomtoa kanga manyoya shingoni . Halafu unakuja na utetezi dhaifu !!

Huyu ni Technically au mwingine?
Ndio maana sisi wengine tunawadharau sana nyie bavicha!

Yani hamjielewi mnasimamia wapi!

Kama sasa hivi hamjulikani mnaunga mkono CCM au mnapinga yani mpo mpo tu!
 
Back
Top Bottom