miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 505
- 941
Ajira ni mahusiano ya bosi na mfanyakazi yaliyofikiwa baada ya Bossi kumhitaji mfanyakazi huyo na kumchukua amtumikie kwa ujira maalum.
Kazi ni shuhuli yoyote ya halali ambayo mtu anaweza kuifanya ili kuongeza thamani ya kitu, ya jambo ama yake yeye mwenyewe bila kujali ina malipo ama haina.
Tatizo la ajira limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Hii inatokana na mabosi kutoona kama wanahitaji kuongeza idadi kubwa ya watu katika kampuni ama taasisi zao huku wasomi wakiongezeka siku hadi siku.
Bahati mbaya sio kwamba hawa mabosi hawana kazi katika makampuni ama taasisi zao ila ni kwamba hakuna bosi anaetaka kuongeza garama bila ongezeko la kipato cha kampuni yake.
Hii ina maana kuwa kama utaweza mshawishi bosi kuwa wewe unaweza kutatua changamoto flani ya kampuni yake kwa kutumia mbinu kadhaa na kampuni hiyo ikastawi zaidi basi kuna uwezekano mkubwa sana huyo bosi akakupa kazi hiyo bila kusita.
Ili tufikie huko lazima tujitahidi sana tusome sana tuongeze ujuzi. Yapo makampuni yanayofilisika kwa kukosa watu wenye uwezo wa kuyakomboa. Sasa kazi ni ya kila anaetaka kazi kujinoa na kujiongezea uwezo wa kutatua matatizo.
Hebu fikiri leo hii uje kwangu uniambie ebwana kuna fursa ya kupanua biashara yako kwa kufanya mambo A, B, C. Kisha ukasema wewe upo tayari kuongeza mauzo yangu na kwa kila utachouza nikulipe kiasi flani. Ntakuwa mjinga kiasi gani kukukatalia?