Kwa mtindo huu Afrika kusonga mbele kamwe ni nadra!.

Kwa mtindo huu Afrika kusonga mbele kamwe ni nadra!.

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Kwa mtindo huu wa kiongozi yupo ukumbini anahutubia ila huko barabarani maisha hayaendelei ni nadra Tanzania kufika uchumi wa kati, ile mnayoitangaza kila wakati huwa ni chengatu.

Yaani hata nyie viongozi mnapokuwa kwenye shughuli zenu za kikazi mjue mnatesa na kuwapotezea raia muda.

Naelekea kanda ya ziwa nimefika Nzega nakutana na msululu wa maroli kama 50 yamesimama, sikuuliza kwa nini wamesimama hapo.

Nilipofika Tinde nakutana tena na msululu wa maroli machache na mabasi yamesimama, ndipo nimeuliza sababu ya kusimama naambiwa 'eti makamu wa Rais sijui yupo wapi huko anasubiliwa kupita.

Hii siyo sawa hata kidogo, mpaka leo mwaka 2022 kiongozi unaruhusu wananchi kusimama wasiendelee na shughuli zao kisa unapita, bullshit!.
 
Kwa mtindo huu wa kiongozi yupo ukumbini anahutubia ila huko barabarani maisha hayaendelei ni nadra Tanzania kufika uchumi wa kati, ile mnayoitangaza kila wakati huwa ni chengatu.

Yaani hata nyie viongozi mnapokuwa kwenye shughuli zenu za kikazi mjue mnatesa na kuwapotezea raia muda.

Naelekea kanda ya ziwa nimefika Nzega nakutana na msululubwa maroli kama 50 yamesimama, sikuuliza kwa nini wamesimama hapo.

Nilipofika Tinde nakutana tena msululubwa maroli machache na mabasi yamesimama, ndipo nimeuliza sababu ya kusimama naambiwa 'eti makamu wa Rais sijui yupo wapi huko anasubiliwa kupita.

Hii siyo sawa hata kidogo, mpaka leo mwaka 2022 kiongozi unaruhusu wananchi kusimama wasiendelee na shughuli zao kisa unapita, bullshit!.
Wafalme wanapita bladifaken
 
IMG_20221122_145948.jpg

Nimeshindwa kupata picha nzuri kwa wale wanaopenda kuona, ila hapo ni kwenye kipima uzito wa magari (mizani) tinde.
 
hawajali kabisa, mimi nilisimamishwa manyoni rais akiwa ndo anaondoka dodoma, alipofika manyoni akaingia halmashauri na sisi tukaendelea kuzuiwa kusubiria apite, nikajikuta najiuliza hivi hii nchi ni yangu kweli
ukiwauliza wanakuzuia kwanini wanafanya hivyo wanadai ni maagizo toka juu
 
Yaani huu ni uzwazwa mkubwa sana. Alafu anachoendea huko aendako hakina manufaa wala direct effect on people's development.

Hii misafara ya viongozi wakuu ni chanzo cha wazi kabisa kinachopnguza kasi ya maendeleo nchini.
 
Daah poleni sana, najua kero yake.
Yaani kikundi kidogo cha watawala wanaofanya tour zao kwa ajili ya per diem za safari ambazo hazina impact yoyote wanasimamisha wengine wasitembee hadi wao wapite!

Tabia za hovyo na za kishenzi sana hizo tuzikemee kwa sauti kubwa. Kuna watu wanahitaji kuwahi mapema wengine ni wagonjwa wanatakiwa wafike haraka hospitalini n.k

Kodi zetu tunazolipa ndio posho zao na mishahara yao ila wanaona sisi wananchi ni mandezi tu, hii haikubaliki sasa wakome kabisa tumechoka, tumechoka, tumechoka.
 
Hii siyo sawa hata kidogo, mpaka leo mwaka 2022 kiongozi unaruhusu wananchi kusimama wasiendelee na shughuli zao kisa unapita, bullshit!.
Ukiwa rafiki wa watu utapita kila kona kwa amani hata kama ni usiku wa manane, ila kama huwatendei watu haki lazima uishi kama digidigi kuhofia usalama wako
 
Hua wanaua uchumi wa nchi huku wakichekacheka hovyo, watumie helcopter hawajifunzi kwa wenzao wakenya upuuzi huo umeshakwisha watu wanashida zao wengine wagonjwa wewe bila aibu uwasimamishe kisa usibiriwe upite? Ajabu sana hii
 
Yaani kikundi kidogo cha watawala wanaofanya tour zao kwa ajili ya per diem za safari ambazo hazina impact yoyote wanasimamisha wengine wasitembee hadi wao wapite!
Hako kakikundi hakana aya hata kidogo ndiyo maana leo wanatuona wananchi kama mazwazwa!.
 
Back
Top Bottom