Kwa mtindo wa uchezaji wa Haaland, hizi ndizo timu zinazomfaa

Kwa mtindo wa uchezaji wa Haaland, hizi ndizo timu zinazomfaa

Darucha

Senior Member
Joined
Dec 28, 2020
Posts
111
Reaction score
211
Timu hizi zinamfaha Sana jamaa akienda kwenye hizi timu anaenda kuwa straiker mmoja hatari Sana duniani na anaenda kuvunja baadhi ya record za ufungaji wa mabao duniani

1- Chelsea
2- PSG
3- Bayern munichen
4- Man utd
5- Real madrid

- Sijawaweka Liverpool, Man city, Barcelona kwa sababu hizi timu hazitaki striker Aina ya haaland na hata Kama ikitokea jamaa kasajiliwa kwenye hizi timu anaenda kufeli balaa unajua ni kwa nini pep gudiola anamuuanzisha Jesus mbele ya aguero ukiachana na maswala ya umri au Saa nyengine Yuko radhi Benando Silva aanze pale mbele kama false no 9.

Au unajua kwa Nini pep gudiola pale Barcelona alishindwa kuendana na mastraiker hatari ambao dunia iliwatambua kuwa ni Bora kama etoo na Zlatan Ibrahimovic na akaamua awachukue David Villa na Henry Basi sababu kubwa ni hii gudiola anapenda mtu anaecheza pale juu no 9 awe anauwezo pia wa kuchezesha wengine leo hii ukimuambia gudiola firmino na halaand mchukue mmoja nahakika anamchukua roberto firmino yote ni kwa sababu firmino ni mzuri pia kwenye kuchezesha wengine.

Yeye haoni shida kumweka bench straiker ambaye nyie mnaona anafunga Sana na akaamua amuweke yule ambaye anajua kuchezesha timu yote ndo maana nasema halaand hana nafasi pale na msije mkashangaa hata Kama halaand akasajiliwa pale man city akaja kuwekwa bench na bernando Silva au Jesus pale mbele.

- Nakuja upande wa Barcelona halaand akienda camp nou anaenda kuonekana ni mchezaji wa kawaida tu kwa sababu Barcelona na wenyewe hawana utofauti Sana na man city wanataka no Tisa ambaye anaweza kucheza na kuelewana na Messi Kama ulivyokuwa kwa Suarez yaani mtu ambaye anaweza kumchezesha Messi pia. Sio yule ambaye anaweza kufunga magoli mengii pekee halaand ni mzuri kwenye kufunga ndio lakini sio mzuri Sana kwenye kuchezesha wenzake.

- Liverpool pia na wenyewe sio waumini wa kumtegemea Sana no Tisa afunge magoli ndo washinde ndo maana baadhi ya wachezaji kama Danny ings na baadhi ya mastraiker wamekimbia pale hasa Chini ya klopp ambaye anategemea Sana mawinga,mafullbacks,na namba Tisa ambaye ni mbunifu yaani namaanisha namba Tisa ambaye anaweza kuchezesha wenzake.

- PSG, Chelsea, Man utd, Madrid, Bayern ndo chaguo sahihi kwa halaand akitua kwenye hizi timu naona anaenda kuvunja record nyingi sana,
 
huyo ibrahimovic aliyefeli barcelona alisajiliwa na guardiola huyo unayesema havutiwi na namba 9 asiyeweza kuchezesha wenzake.pia guardiola hakuhusika na usajili wa thiery henry.

Guardiola ni muumini mkubwa wa position position position,possession, play. thiery henry aliwahi kutolewa nje kwa sababu ya kuhama position yake licha ya kufunga goli
 
Arsenal mbona hujaitaja lakini? Au unatuonea wivu na unbeaten run yetu ambayo haijavunjwa record pale epl. Arsenal inamfaa zaidi 😎
 
Ao wazeee wa mchakamchaka borosia wanaremba sana.
 
Mimi ni Chelsea, ila namshauri dogo aende Real Madrid ili akachukue ile tuzo ya mchezaji bora wa dunia. Natumaini na Kylian Mbappe nae ataunga tela kuhamia Madrid ili kwenda kukinukisha tena baada ya kuondoka kwa Christiano Ronaldo.
 
Chelsea na Man U ni kama Arsenal zilizochangamka tu, hakuna mtu anazitegemea hizo timu kushinda mataji makubwa kama uefa au prem. Kumaliza top 4 ni kama kushinda taji kwa hizo timu.

Haaland anafaa kucheza timu yenye uhakika wa kushinda ligi ya ndani na kufika angalau nusu fainali ya uefa kila mwaka.

Bayern, Paris, Man City, Real, Barca hizi ndio timu kubwa na zenye ushawishi barani ulaya, timu ambazo kocha kama huleti taji hata moja mwisho wa msimu unatimuliwa.

Man U wanakwenda miaka minne bila kunyanyua chochote na Ole bado yupo yupo tu
 
Chelsea na Man U ni kama Arsenal zilizochangamka tu, hakuna mtu anazitegemea hizo timu kushinda mataji makubwa kama uefa au prem. Kumaliza top 4 ni kama kushinda taji kwa hizo timu.

Haaland anafaa kucheza timu yenye uhakika wa kushinda ligi ya ndani na kufika angalau nusu fainali ya uefa kila mwaka.

Bayern, Paris, Man City, Real, Barca hizi ndio timu kubwa na zenye ushawishi barani ulaya, timu ambazo kocha kama huleti taji hata moja mwisho wa msimu unatimuliwa.

Man U wanakwenda miaka minne bila kunyanyua chochote na Ole bado yupo yupo tu
Kabla ya kuamua usaini wapi kwanza unaangalia iapokwenda kuna nani na mimi nitakaaje. psg kuna neymar na mbape, madrid kuna madogo wanaandaliwa kila mtu ni king, man utd kuna rashford na greenwood na wengine wengi wapo tayari na hawataki kuharibu academy yao.. arsenal anauhakika [emoji817] na kucheza kama striker na kupata mipira yote ashindwe yeye tu, barca kuna ansu fati anaandaliwa kuwa gaucho na messi atabaniwa na atapotea kama coutinho, dembele, griezman. Chelsea anaweza kucheza ila hawezi kushaini timu la kizee na halina mvuto
Bayern kuna sane, mnyama lewandowski
 
Back
Top Bottom