Pre GE2025 Kwa muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu, kauli ya "No reform, No election" ni sawa na kufua kanzu ya kwendea msikitini ijumaa saa 6 na nusu mchana

Pre GE2025 Kwa muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu, kauli ya "No reform, No election" ni sawa na kufua kanzu ya kwendea msikitini ijumaa saa 6 na nusu mchana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Pona ya CCM wananchi wasilielewe ili somo, otherwise naiona serikali isiyokuwa na dhamana ya wananchi Ina ambayo viongozi wake wanafia madarakani hadi akili zitupate. Sisi ni wepesi wa kisahau
 
CCM hata wapewe miaka 100 bado hawataki katiba mpya.
Wanataka viraka kwenye katiba yao ya '77.
Lazima mteme bungo this time.
 
Hakuna mahesabu yoyote ambayo ya naweza kutoa jibu kwamba kwa muda tulio nao, nchi inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kikatiba.
Labda muda kweli ni mfupi, hautoshi...

Lakini ishu kubwa kwenye hili wala sio muda bali ni utashi wa kisiasa...

Nia na utashi wa kuona tatizo ukiwepo na kisha tukaamua sote kama taifa kukaa chini ili kuona tunakwendaje mbele kwa pamoja kwa kuondoa au ingalau kurekebisha baadhi ya mambo ya msingi yanayolalamikiwa, basi unaweza kuona kwa uwazi kabisa kuwa, ishu ya muda wala si kitu na sio tatizo hata kidogo..

Kwa mfano, kwani kuna ubaya gani iwapo stakeholders wote tukikutana na kukubaliana kuwa;

"...Ok, muda hautoshi, tufanyeje? Je, tusukume mbele uchaguzi ili tushughulikie kasoro hizi? Au tufanye marekebisho gani madogo yanayoweza kufanyika sasa ili kurudisha imani kwa wananchi na kila pande ziwe comfortable kuingia kwenye uchaguzi? Mfano, kurekebisha tatizo la mgawanyo wa majimbo kwa usawa unahitaji muda gani? Kurekebisha sheria ya kuipa mamlaka kamili ya uhuru NEC ili isimamie uchaguzi unahitaji muda gani kama sio kupeleka sheria tu bungeni na kufanyiwa marekebisho? Kufanya ammendments ndogo kwenye katiba ili kuruhusu uchaguzi huru, wa haki na wa wazi unahitaji muda kiasi gani eti..."

Kwenye hili, ishu sio muda Ndugu chiembe. Ishu ni LACK OF WILLINGNESS ya kufanya mabadiliko haya...!

Watu wakikaa pamoja wakiwa na mioyo safi isiyo na hila ndani yake ili kutatua tatizo fulani, basi, tatizo hili hutaturika pasipo kusababisha madhara kabisa na amani ikaendelea kutamalaki....

Kwa hiyo, mimi narudia tena kusema, tatizo hapa sio muda bali ni kutokuwepo kwa utashi wa kisiasa toka kwa wenye mamlaka ya maamuzi na kwa sababu wanasubiri mpaka circumstances iwashurutishe kufanya yale wanayopaswa kuyafanya wakati hawako under pressure...
Tunajua Lissu na genge lao wana kiu kali ya madaraka wakiamini watakuwa matajiri kwa kutumia fedha za umma.
Huu sasa ni ujinga ulio wazi sana ktk mawazo yako..!!

Hizo pesa za umma za kuwatajirisha kina Tundu Lissu wazitoe wapi wakati hawana serikali..?

Nyie CCM mlioko serikalini na wenye serikali ndiyo mko accountable na kila senti ya fedha za umma maana ndiyo wenye mamlaka ya kuzikusanya, kuzipangia matumizi na ikibidi kuzifisadi ili mjitajirishe sawasawa na mawazo yako haya...

Sasa hebu niambie, mlango wa kuingilia kina Tundu Lissu ili wachukue hizo pesa za umma uko wapi..?
Lakini huwasikii wakiongelea maendeleo ya mwananchi. Wao ni vita ya madaraka tu.
Ni ujinga na hila tu zinakusumbua ndugu chiembe ..

Ukielimishwa huo ujinga utakutoka, utaelewa na utakuwa si mjinga tena, bali mtu mwerevu unayeelewa...

Kaulimbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION in facts ni ufunguo wa maendeleo ya wananchi...

Au hujui kuwa tuliambiwa ili nchi iendelee inahitaji mambo manne muhimu yafuatayo?:

➡WATU

➡ARDHI

➡SIASA SAFI na

➡UONGOZI BORA..?

Hayo mawili ya mwanzo, hayana shida. Shida iko kwenye hayo mawili ya mwisho; ukosefu wa SIASA SAFI na UONGOZI BORA katika nchi na taifa letu. Nchi na taifa letu lina "BORA VIONGOZI" hatuna "VIONGOZI BORA..."!

Mathalani, inawezekana vipi kuwa na viongozi bora iwapo michakato ya kisiasa ya kuwapata viongozi hao bora iko so corrupt & compromised...?

Utapataje maendeleo iwapo viongozi wanajiweka wenyewe kwenye nafasi za kuongoza watu kwa njia za mabavu na rushwa pasipo ridhaa ya waongozwa...??

Hii kauli mbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION lengo lake ni kuondoa uchafu huu ili kuweka mazingira yaliyo huru na salama ya watu kujiletea maendeleo yao na kuwa na viongozi wanaowajibika kwa umma kwa kuhakikisha hawawaibii wananchi rasrimali zao....

Hali ilivyo sasa ni mbaya mno, inahitaji marekebisho..
Nchi iende kwenye uchaguzi, haya mengine yataongeleka katika muafaka mwaka 2026
Haitakuwa hivyo...

Kama tukikaa chini, tukaliona tatizo kwa pamoja na kukubaliana kuwa ni kweli tunahitaji kufanya mabadiliko ya kisheria na kikatiba ili kuruhusu chaguzi huru, za wazi na za haki kwa kila mtu na kukubaliana njia ya salama ya kupita ili kuyafikia mabadiliko haya, kila kitu kinawezekana....

Na ikiwa tutaona muda ni kweli mfupi hautoshi kiasi cha kuwezesha uchaguzi wa mwaka huu 2025 kufanyika, basi hakuna ugumu wowote wa kukubaliana kuusukuma uchaguzi mbele ili kuruhusu reforms hizi muhimu kufanyika kwanza..

Hilo☝🏻☝🏻 ndilo linalowezekana sasa na sio hilo jingine ambalo lina hila ndani yake...!!
 
La kusogeza uchaguzi mbele ni kuwatoa kwenye ramani watu wanaojipanga kugombea kupitia chadema, ni kuwazubaisha
Hakuna mwenye moto na chaguzi za kishenzi boss.
 
Muda umekwisha, shiriki uchaguzi au acha, habembelezwi mtu hapa
Wewe si ukae huo mkao?lala usingizi ,amka fanya unalodhani Lina manufaa kwa kizazi chako.Nchi ni zaidi ya shibe yako ya Leo..!
Kama unalipwa kufanya propaganda zako,sawa,ila kama ndio uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho,jitafakari .
Ni choice tu lkn.
 
Utajua hujui. Mwaka huu yatafanyika mambo makuu ambayo hayajawahi kufanyika tangu kuzaliwa kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom