Kwa mujibu wa cheo chake ndani ya CHADEMA, sasa Halima Mdee atakuwa Bungeni kama Mbunge Huru. Tutarajie nini?

Kwa mujibu wa cheo chake ndani ya CHADEMA, sasa Halima Mdee atakuwa Bungeni kama Mbunge Huru. Tutarajie nini?

dikteta2020

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
595
Reaction score
3,991
CHADEMA inakidhi vigezo vya kupata uwakilishi wa viti maalum maana imepata zaidi ya asilimia 5 ya kura za ubunge.

Kutokana na muongozo liwake jua ama mvua Josephati Gwajima anaenda kukutana na Halima Mdee Bungeni kama Mwenyekiti wa BAWACHA. Mbaya zaidi atakuwa mbunge huru asiye na jimbo la kusemea sijui maji au madawa. Wakati Gwajima atakapokuwa akilalamikia mafuriko, Mdee atakuwa akilisemea taifa pamoja na hayo mafuriko atakayokuwa akilalamikia Gwajima.

Aisee muda wa Gwajima bungeni utakuwa mchungu sana.

Pamoja na yeye pia watakuwepo wanawake wengine machachari. Akiwemo Agnesta Lambart, Lucy Mgabe nakadhalika.

Any way acha tuanze kwanza maandamano ya kudai haki na mimi nitashiriki
 
Mhh! Hamna kitu kama hicho, viongozi wako wameshinikiza walioshinda wasikubaliane na uchaguzi kwa hiyo hata hiyo asilimia tano sahau
 
Unaona sasa hawa jamaa walivyokuwa wabinafsi? Yule dada Rukwa aliyeshinda wamemshinikiza akatae Ubunge wake alioupigania na kuusotea kwa jasho na kufanikiwa kuwashawishi Wananchi wamchague huku yeye Halima Mdee aliyekataliwa na wananchi anaenda (anataka) Bungeni kupitia mlango wa nyuma, why? Why, man so selfish?
 
Gwajima tatapata full support ya serikali batili ya Magufuli, amewekwa hapo kulinda mali za familia zilizomo Kawe. Ikiwa ni pamoja na viwanja vya unonio.
 
Kushiriki katika hilo Bunge ni kuhalalisha ubakaji wa demokrasia uliofanyika.
Mkuu subiri utaona maajabu, CHADEMA itawateua viti maalum na bungeni wataenda. Mmoja wa wataoenda ni Halima Mdee
Ndio maana muda mwingine tunapaswa kuelewa kuwa wanasiasa hawako serious kihivyo kama tunavyodhani.
 
Hakuna haja ya CHADEMA na ACT kupeleka wabunge. Huo utakuwa ujinga. Viongozi wamekwishasema hilo. Akakutane na Gwajima ili iweje? Bunge la shetani hilo wamwachie shetani na nduguze (CUF).
Tatizo lenu mnashindwa kuelewa siasa na wanasiasa.
CHADEMA itateua viti maalum na wataenda bungeni, haya mengine yatapita tu kama kawaida, sihitajin tubishane kwenye hili ila subiri.
 
Kwani alivyokuwa mbunge zaidi ya miaka 10, alikuwa anasemaje? Hivi CHADEMA hakuna watu wengine tofauti na kina Mdee, Sugu, nk. Hata sishangai Mbowe kuwa mwenyekiti wa maisha!
 
CCM msitake ushirika na CHADEMA ktk batili yenu. Hakuna mwanachadema yeyote akayekuja bungeni. Kuanzia kesho ni full maandamano mpk uchaguzi urudiwe.
 
Acheni kujifurahisha. Yule mwizi na mzandiki aasiye na huruma wala utu atupishe.
 
Si tulisikia mmewaambia wabunge wenu waliochaguliwa wajitoe, vipi tena? Njaa mbaya sana, saivi hadi mbowe anatamani na yeye aingie bungeni kwa viti maalumu
 
Unaona sasa hawa jamaa walivyokuwa wabinafsi? Yule dada Rukwa aliyeshinda wamemshinikiza akatae Ubunge wake alioupigania na kuusotea kwa jasho na kufanikiwa kuwashawishi Wananchi wamchague huku yeye Halima Mdee aliyekataliwa na wananchi anaenda (anataka) Bungeni kupitia mlango wa nyuma, why? Why, man so selfish?

chama cha kipuuzi sana hiki,
 
Si tulisikia mmewaambia wabunge wenu waliochaguliwa wajitoe, vipi tena? Njaa mbaya sana, saivi hadi mbowe anatamani na yeye aingie bungeni kwa viti maalumu

hahaha daaah mbavu zangu
 
Aendelee kukoroma , kuandamana.
Akifia selo anakifia chama chake.
Wana Kawe Halima hatuhusu tena.
 
Kwanza kwanini Halima anapewa kipaumbele,kwanini asiwe Bulaya, Matiku au mwingine?
Lakini wametoa tamko la kususia izo nafasi za Udiwani na Ubunge, nina mashaka na huo msimamo wakususia, labda kama mwenyekiti wa chama angekuwa Lissu, ila kwa Mbowe piga uwa atabadili gia angani ili aendelee kuwachangisha fedha wabunge watakao ingia Bungeni.
 
Unaona sasa hawa jamaa walivyokuwa wabinafsi? Yule dada Rukwa aliyeshinda wamemshinikiza akatae Ubunge wake alioupigania na kuusotea kwa jasho na kufanikiwa kuwashawishi Wananchi wamchague huku yeye Halima Mdee aliyekataliwa na wananchi anaenda (anataka) Bungeni kupitia mlango wa nyuma, why? Why, man so selfish?

Halima ni mwanamke.
 
Kwanza kwanini Halima anapewa kipaumbele,kwanini asiwe Bulaya,Matiku au mwingine?
Lakini wametoa tamko la kususia izo nafasi za udiwani na ubunge,minamashaka nahuo msimamo wakususia,labda kama mwenyekiti wa chama angekuwa Lissu,ila kwa Mbowe piga uwa atabadili gia angani ili aendelee kuwachangisha fedha wabunge watakao ingia Bungeni.

Jitahidi ujifunze kuandika vema, sio wote ni wajinga wenzio wanaosoma hapa!
 
Back
Top Bottom