Mwanachama Tlaatlaah anachukiwa na kukosolewa vikali na sehemu kubwa ya watumiaji wa JamiiForums kutokana na mambo makuu yafuatayo: [1, 2]
Kuitwa "Chawa" na Propaganda za Kulipwa: Wakosoaji wake wanadai kuwa haandiki kwa utashi wake bali analipwa kutetea serikali na chama tawala cha CCM. Mara nyingi kwenye nyuzi zake hutumia lugha ya Kiingereza au Kiswahili cha kusanifika sana kusifia viongozi, jambo linalofanya wengine wamuone kama mtu anayeendesha kampeni maalumu ya kisiasa (propaganda) badala ya mijadala huru. [1, 2, 3, 4]
Kupuuza Changamoto za Uhalisia za Wananchi: Analaumiwa kwa kutokuwa na uhalisia (out of touch) na maisha ya kawaida ya Watanzania. Hata kukiwa na malalamiko ya dharura kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, masuala ya katiba, au kero za kijamii, yeye huendelea kuposti takwimu za ukuaji wa uchumi na miradi ya serikali akionyesha kana kwamba kila kitu nchini kiko shwari kabisa. [1, 2, 3]
Mashambulizi ya Mara kwa Mara Dhidi ya Upinzani: Huwa anaanzisha nyuzi nyingi zinazolenga kuushambulia, kuudhihaki au kutabiri kusambaratika kwa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA na viongozi wake kama John Heche au Tundu Lissu. Hili linamfanya kuwa adui mkubwa wa wafuasi wa vyama hivyo jukwaani. [1, 2]
Ukurasa wake Kufurika Nyuzi Zisizo na Uhakika (Uzushi): Mara nyingi hushutumiwa kwa kueneza uvumi au propaganda zenye mrengo wa kisiasa ili tu kuwachafua wale wasio na msimamo sawa na serikali au CCM. [1]Ushirikiano wa "Kichawa" (Syndicate): Wanajukwaa wanachukizwa na mtandao wake na wanachama wengine wenye tabia kama yake (kama Lucas Mwashambwa). Huwa wanajazana kwenye nyuzi zao wenyewe kusifiana, jambo linaloboa watumiaji wanaotafuta mijadala yenye fikra tunduizi na hoja zenye mashiko. [1, 2, 3]
ngoja kwanza ncheke
Aise Google ni waongo sijawahi kuona
yaani,
Tlaatlaah kufanya kazi ya kizalendo ya kueleza ukweli mtupu kwenye mambo ya msingi tu kitaifa na kimataifa,eti analipwa? dah 🤣
na mbona hawajasema nalipwa na nani, kiasi gani na kwa bank account ipi?
Let me help them,
silipwi na yoyote hata senti moja, na si hitaji kulipwa kwasababu,Neema na Baraka za Mungu zanitosha.
Yes,
naweza kua na chukiwa, but myself, ninawapenda waTanzania wote regardless ya chuki au mihemko yao useless dhidi yangu, but I love them to the maximum and tirelessly, I will continue fighting for them with all my heart, against all enemies that endengerz our unity, peace, security and stability of our beautiful nation, Tanzania.
You know,
nonsense narratives like chawa, nyumbu, wafuata mkumbo and the like, have completely no impacts as far as politics is concerned. So, to me, those useless narratives are just hot air, they can not stop me from expressing my free political views in Jf.
Lakini pia,
niwasaidie Google kidogo kwamba, binafsi sishinikizwi na yoyote kuandika chochote jf, bali ninaandika kwa utashi na akili yangu mwenyewe kama wadau wengine wa Jf.
Lakini pia,
nimekwenda shule, na nina elimu ya juu. Ninajua kusoma na kuandika vizuri sana lugha ya kiswahili, kiingereza na Kiarabu ingawa naweza kukosea mara chache chache kwasababu ni lugha nilizojifunza tu, na ninapenda kuzitumia kwa pamoja ikiwa najiskia kufanya hivyo.
Suala la kusanifu ni la kawaida tu inapobidi kufanya hivyo, ingawa binafsi sipendi.
Jambo lingine muhimu ambalo ningependa kueleza kinagaubaga ili kuondoa upotoshaji wa Google na baadhi ya wadau wa Jf dhidi yangu ni kwamba,
Si kweli kwamba,
eti mimi napuuza uhalisia wa changamoto za wananchi. Huu ni uongo na upotoshaji mkubwa dhidi ya wajibu wangu dhidi ya masuala yanayohusu na kugusa maisha yao. Mimi ni kiongozi wa wananchi, na mimi ni mtetezi wa wananchi, in fact, uchapakazi wangu na weledi wangu katika kuwatumikia wananchi ndio umenifikisha hapa nilipo hivi sasa. Heshima niliyonayo hivi sasa kitaifa na kimataifa inatokana na mimi kujali zaidi maslahi mapana ya waTanzania wote.
Kwahiyo Google ni wapotoshaji.
Mimi daima hupuuza porojo, uzushi na uongo useless wa kutafuta kiki na public sympathy jukwaani. Na kabisa siwezi kuvumilia kuona nonsense kama hizo zikitrend jukwaani. Nitaendelea kuwatetea wananchi kadiri niwezavyo mpaka pale mambo yao yakae sawa.
Kwenye hili la kukichukia chadema na viongozi wake,
pia naomba niwasaidie Google.
Kwanza mimi siichukii chadema wala viongozi wake hususani fisadi heche na kibaraka Lisu. Hawa majamaa ni marafiki zangu sana. Wakiwa wabunge tumekutana sana casino na kuinjoy pamoja. Tumeshauriana na kusaidiana mambo mengi sana kama ndugu. In fact, bado tunawasiliana na tunaheshimiana sana. Na siasa haijawahi kutufanya kua maadui wala kuchukiana.
Halafu Google,
mimi kama mtaalamu mwandamizi katika siasa nawezaje kukichukia chama cha siasa ambacho hakina hata sifa za kisheria kushiriki uchaguzi? Acheni uongo bana. Chadema ndio haswa wanavichukia vyama vingine vya upinzani but not me.
Mwisho,
niwahakikishie tu waTanzania wote kwamba, ni vizuri kupuuza upotoshaji wa Google dhidi ya wadau mbalimbali wa JF, lakini pia niwahakikishie kwamba binafsi nitaendelea kueleza ukweli mtupu kwenye mambo ya msingi tu humu jukwaani, regardless ya mihemko, chuki au makasiriko ya baadhi ya wadau useless wa jf lakini pia bila kujali porojo za Google.
Nipo jukwaani la siasa kufanya siasa na sio kuhubiri injili.
Mjulishe na mwenzako kuhusu haya 🐒