Mwanzo, nilidhani utakua uzushi, ila leo kupitia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM, ndio nimeamini kupitia matamshi yake. Hv ni kwanini Ndg. Mrisho Kikwete huwa hataki kutamka Jina "Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere"????
Je na zile picha za kumbukumbu zenye Jina la Baba wa Taifa..., ziliandikwa kimakosa??
By bullet proof:
Nimewahi kusikia kwa mtu kuwa Rais Kikwete huwa hamuiti Mwalimu Nyerere 'baba wa taifa', kama tunavyofanya watanzania wengi. Japo sina uhakika sana na hili, mimi pia nimemsikiliza JK mara kadhaa anapoongea kuhusu Nyerere hamuiti baba wa taifa bali humuita 'mzee Nyerere'.
Kuna sababu yoyote ya maana inayomfanya JK asimuite baba wa taifa? au ameamua mwenyewe tu kumuita hivyo? Kuna tatizo lolote kutokumuita baba wa taifa?