Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2020 Jeshi la Polisi lilitajwa kama kinara wa Rushwa Tanzania

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2020 Jeshi la Polisi lilitajwa kama kinara wa Rushwa Tanzania

Mfilipi WaTanzania

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
3
Reaction score
6
Kwa Mujibu wa Utafiti wa “National Governance And Corruption Survey 2020” Jeshi la Polisi ni Taasisi Kinara kwa Rushwa nchini Tanzania kwa tasisi za Umma ikiwa na Alama 45.6%.

Huu ni Utafiti uliofanywa kwa kuhoji Wananchi Maeneo Mbalimbali nchini. Wahojiwa walitoa maoni na kuonyesha kuwa Jeshi la Polisi ni Kinara Kwa rushwa katika kutekeleza Majukumu yake.

Kwa Maisha halisi ni wazi kuwa jeshi la Polisi hasa idara ya usalama barabarani bado ni pasua kichwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa maeneo mengi nchini kwa mjini na vijijini. Jeshi hili lenye dhamana ya kulinda amani ya wananchi na Mali zao linapaswa kuwa na njia bora zinazozingatia uadilifu, uwajibikaji na nidhamu ili kuweka Imani kwa wananchi na kukuza uzalendo kwa taifa letu.

Askari wanaobainika kushiriki vitendo vya rushwa wanapaswa kuchukuliwa hatua Kali ili kuwa fundisho kwa wengine na kulinda heshima ya Jeshi la polisi. Mwisho Kabisa, hatupaswi kufichana kwa maovu yanayohatarisha ustawi wa taifa letu kwa kuongea mabaya hayo kwa maneno bali kuyatatua na kumaliza kabisa.

@polisi.tanzania @policetanzania @jeshi_la_polisi_tanzania

Blue and Yellow Modern Did You Know with Circle Frame Facebook Post_20240712_153445_0000.png
 
Back
Top Bottom