Kwa muonekano M23 ni jeshi la nchi fulani

Kwa muonekano M23 ni jeshi la nchi fulani

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Rwanda ya kagame inacheza game moja chafu sana eneo la maziwa makuu.

Kwanza walipovamia congo walipandikiza majasusi kibao congo. Jeshi la DRC Fardc si chochote ni mkusanyiko wa wahuni tu. Nimeambiwa na marafiki majenerali wanajichubua ngozi na wanajaa kwenye mabaa kustarehe tu. Hawana weledi wamekalia kupokea maelekezo toka rwanda kwa ujira.

Ndio maana Fardc ni kukimbizwa ovyo na M23 bila hata kufyetua risasi.

Mchezo anaocheza kagame congo ni utumishi kwa makampuni yanayopora madini ya Congo ambapo rwanda na uganda ni wabia. Inaelekea baadhi ya viongozi DRC na Makamanda wa Fardc wanahusika. Munusco vikosi vingi ni kutoka india na pakistan. Hawa nao penye madini usifikiri watapigana na mtu mwenye madini.

JWTZ walishatoa mchamgo kuwapiga na kuwafukuza hadi Uganda hao M23. Hebu fikiri kwa nini uganda isihakikishe kikundi hicho kinakufa? Badala yake wamekilea hadi kuweza kurejea tena.
 
Hapa tunamtegemea Msuya na cdf mpya kupitia MI bàsi.
 
M23 wana latest weapons from USA, Germany & UK.
Zinaingiaje na zinapita wapi?

Hii vita Jeshi la DRC haliwezi kuishinda
 
Mchezo mchafu ndio zake na hata baadhi ya captains wa vikosi ni toka nchini mwake..Yuko makini na muonekano
 
M23 wana latest weapons from USA, Germany & UK.
Zinaingiaje na zinapita wapi?

Hii vita Jeshi la DRC haliwezi kuishinda
Hizo ndio propsganda za kisaikolojia hawa watutsi wanapiga kwa mafanikio dhidi ya wakongo.
M23 ni wepesi. Msisahau jwtz waliwadunda hawa na kuwavurunisha hadi kutokomea uganda japo wakongomani wanaambiwa jeshi lao hili la waoga ndio waliwapiga M23. Jambo la kusikitisha ni kwa nini uganda wamewalea m23 hadi sasa wanafanya uvamizi tena congo.
 
Dawa ya Kagame inachemka na wanayo wahutu. Ni suala la muda watarudi na kumaliza game. Kwa anayejua historia ya jamaa hawa, never say never. Hata Kagame na wenzake wanalijua hilo.
Huo ndio ukweli wenyewe, Mwisho wa familia ya huyu tall man itakuwa ni kuwa exiled from their own land kwenda kuishi baba yao anakopeleka mboga saizi… stori haitatofautiana sana na kwa jirani yake Kaguta… time will tell….
 
Ni vizuri ieleweke, RPF na M23 ni baba na mwanae. Ifahamike pia M7 na tallman lengo lao linafanana, wanaiwinda A.mashariki kwa ujasusi wa hari ya juu mno japo tunaona kama mzaa hivi lakini wana majasusi hatari sana hata bapa Tz majasusi wa Tall man ni wengi huwezi amino ..wanafanya nini na wanataka nini? utajua mwenyewe. Ndoto ya Tallman bado iko, one day anakuwa juu ya A. mashariki.

Msisahau, mpango wao ilikuwa kila baada ya miaka 10 lazima mapinduzi, huu mpango upo na haujaisha japo hapo juzi jamaa baada ya kugundua nchi iko mateka ilibidi mbinu mbadala itumike akasafiri kwa miguu toka Tz hadi Bujumburu ndo akatangaza nchi iko salama, lakini bila JWTZ alishapakatwa yule

Kwa kifupi, historian ya hapa A. mashariki ya kati haina tofauti sana na ile ya ukanda wa Gaza na mashariki ya kati, zote ni za muda mrefu na zote zina historia yenye mizizi. Usiwasahau akina Ndadaye, Buyoya n.k

Yule dogo juzi alichokisema kuhusu Kenya alafu baba akampandisha cheo mnakikumbuka? Endeleeni kukesha baa na balaa litawakuta huko baa
 
Hata kule msumbiji ni huyohuyo kagame hamna lolote! Wange mpoteza tu kagame hatufai kabisa east africa green snake in a green grasses
 
Hata kule msumbiji ni huyohuyo kagame hamna lolote! Wange mpoteza tu kagame hatufai kabisa east africa green snake in a green grasses
Binafsi natia shaka sana ushiriki wa rwanda msumbiji. Badala ya kufanya kazi na msumbiji wanaweza kufanya kazi na wawekeza wa gesi na mafuta kwa ujira au kufanya shughuli kama mamluki kulinda wahujumu kwenye madini. Ilkua makosa msumbiji kuita rwanda. Chanzo cha kuihujumu congo hawakutaka kuondoka walipotakiwa. Pia raia wa rwanda walidai vyeo vikubwa nchini congo kama vile ni rais.
 
Kagame hutumia muda mwingi kuwahujumu marais wasiojielewa. Jpm alipogundua kuwa kagame si mzuri alikata mawasiliano haraka sana. Jk pia alikuwa smart sana kudeal na huyu myahudi feki wa kigali.
 
Kagame hutumia muda mwingi kuwahujumu marais wasiojielewa. Jpm alipogundua kuwa kagame si mzuri alikata mawasiliano haraka sana. Jk pia alikuwa smart sana kudeal na huyu myahudi feki wa kigali.
Wacha uwongo wako huyo jamaa na JPM walikuwa damdam. Kidole na pete.
 
Back
Top Bottom