Kwa mustakabali wa Elimu:Hili nalo tuliangalie....

Chipolopolo

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2012
Posts
1,425
Reaction score
726
Kuanzia mwaka huu mtihani wa kidato cha pili umerejeshwa kwa lengo la kuchuja watakao ingia kidato cha tatu wawe wamefikia kiwango fulani cha ukomo wa alama za ufaulu.Mpango huu umeingizwa katika utekelezaji bila maandalizi ya kutosha.

Hadi sasa kuna shule hasa za kata ambazo hawana kidato cha tatu mwaka huu kutokana na kukosa alama stahili.Hata hivyo changamoto nyingine ni hii: Mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili (sasa cha tatu ) alipata alama alama C kwa masomo yote yanayo itwa arts.

Physics alipata 49 na Chemistry 33.Mathematics 21 na Biology 21. Kwa mfumo wa elimu tulio nao,mwanafunzi huyu amepangiwa kusoma masomo ya arts.Ameelekezwa kuacha Physics na Chemistry.Lakini analazimika kusoma Biology na Mathematics ambayo katika nadharia ya kawaida hakufaulu kwa kiwango kizuri kulinganisha na masomo aliyo elekezwa kuyaacha.Ni rahisi kubashiri kwamba matokeo yake ya kidato cha nne yanaweza kuwa mabaya.

Analazimika kusoma asichoweza.Ama sivyo angetakiwa kusoma masomo yote.Kwa hili na mengine: Nini kifanyike katika kuokoa elimu yetu kwa faida ya watoto wetu na taifa kwa ujumla?
 
Sasa Chipolopolo kama mtoto anayeingia kidato cha kwanza hajui kusoma na kuandika akiifika kidato cha pili atakuwa amejua?Na kama amejua nawezaje kufuatilia masomo ya sekondari ilhali yale ya primary hayajui?

Tuanzie na elimu ya walimu wetu wanaofundisha shule za msingi wawe wa daraja gani?Na je mwanafunzi aliyepata div.IV anaweza kumfundisha mwenzake wakati shule imeshinda?

Kwa nini tusiipigie kelele serikali vile vyuo binafsi na vya serikali viache kuanzia sasa kupokea wanafunzi waliofelie kidato cha nne kwenda kuwa waalimu

Na mwisho walimu pigeni kelele sasa walimu wa vodafasta wanawavunjia heshima yenu.
 

Tetty: Uko sahihi. Lakini bado utaona kunashida pia katika maamuzi hayo. Aliyefaulu vizuri ni ni nadra kwamba atapenda kuwa mwalimu katika kiwango cha shule ya msingi au sekondari.Kwa sababu alama zake za ufaulu zitampa nafasi ya kuchagua fani ambayo itamlipa zaidi kuliko hii tunayosema ualimu ni wito.Iwapo wataboreshewa mishahara itawashawishi hata wenye vipaji maalumu kusomea ualimu. Kinyume chake ni vigumu.

Vile vile: tazama mfumo wetu wa elimu. Unamtambua hadi mwenye IV-33 kwamba amefaulu. Lakini kiuhalisia hakuna chuo chochote kinachoweza kumchukua. Mpaka hapo kuna maana gani kumtambua huyo mwenye IV kuanzia, kwa mfano 27-33 kuhesabika amefaulu? Changamoto bado tunayo....

Kwa nini tusiipigie kelele serikali vile vyuo binafsi na vya serikali viache kuanzia sasa kupokea wanafunzi waliofelie kidato cha nne kwenda kuwa waalimu

Na mwisho walimu pigeni kelele sasa walimu wa vodafasta wanawavunjia heshima yenu.[/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…