Chipolopolo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 1,425
- 726
Kuanzia mwaka huu mtihani wa kidato cha pili umerejeshwa kwa lengo la kuchuja watakao ingia kidato cha tatu wawe wamefikia kiwango fulani cha ukomo wa alama za ufaulu.Mpango huu umeingizwa katika utekelezaji bila maandalizi ya kutosha.
Hadi sasa kuna shule hasa za kata ambazo hawana kidato cha tatu mwaka huu kutokana na kukosa alama stahili.Hata hivyo changamoto nyingine ni hii: Mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili (sasa cha tatu ) alipata alama alama C kwa masomo yote yanayo itwa arts.
Physics alipata 49 na Chemistry 33.Mathematics 21 na Biology 21. Kwa mfumo wa elimu tulio nao,mwanafunzi huyu amepangiwa kusoma masomo ya arts.Ameelekezwa kuacha Physics na Chemistry.Lakini analazimika kusoma Biology na Mathematics ambayo katika nadharia ya kawaida hakufaulu kwa kiwango kizuri kulinganisha na masomo aliyo elekezwa kuyaacha.Ni rahisi kubashiri kwamba matokeo yake ya kidato cha nne yanaweza kuwa mabaya.
Analazimika kusoma asichoweza.Ama sivyo angetakiwa kusoma masomo yote.Kwa hili na mengine: Nini kifanyike katika kuokoa elimu yetu kwa faida ya watoto wetu na taifa kwa ujumla?