jojipoji koromije
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 1,127
- 1,635
Wana bodi sasa ifike Mwisho!!
Nchi inapaswa kubadilika katika mfumo wa bunge ili kuwe na watu mahiri na werevu na wenye elimu ya kung’amua mambo mazito ya kuendesha Nchi. Sikatai Wananchi kumchagua mgombea kama Baba level, Msukuma na wengine kama akina Tabasamu na Shigongo kuwa wawakilishi wao.
Ni haki yao kabisa. Lakini hawa maamuzi yao yanapaswa yakomee huko chini; bila kuathiri mwenendo wa uelekeo wa Uchumi, Uongozi katika ngazi mbalimbali (Uteuzi wa nafasi nyeti), upitishwaji wa sheria na miswada nyeti kwa maslahi mapana ya Nchi.
Sasa hapa ndo kunakuja umuhimu wa kuwa na Bunge la Seneti ambao wabunge hawa wanapaswa kuwa na sifa mahiri katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, Kijamii, kimaendeleo, kielimu nakadhalika. Seneti ndo itakuwa na mamlaka ya kumwajibisha Rais Au Waziri na viongozi wengine watakaokiuka Miiko ya uongozi.
Ni aibu sana na fedheha kuamuliwa mustakabali wa Taifa na watu ambao hawana weledi, hawajasoma, na wanaobahatisha katika maisha bila kuwa na nia ya dhati. Kweli tunahitaji mabadiliko namna ya kuwa na Bunge Bora zaidi. Hatuwezi baki kule kule kwa Mwaka 1961.
Ili kufikia maendeleo ya kweli tusiangalie gharama, ni wakati sasa wa kutengeneza Tanzania 🇹🇿 iliyobora kwa kizazi cha sasa na kijacho.