Kwa mwenendo huu, siku moja serikali ya Tanzania itakuwa ya kijeshi

Kwa mwenendo huu, siku moja serikali ya Tanzania itakuwa ya kijeshi

Wakuu, kwa hali ya kisiasa ya style hii katika nchi, kuna harufu pengine jeshi lililo upande wa wananchi likaingilia kati, ipo siku tutalala tukiongozwa na Rais tunayemjua tukaamka na mamlaka ya kijeshi kama ilivyo huko 🇧🇫, 🇲🇱 na 🇳🇪.
Bora iwe hivyo maana wakina tlaatlaah,chiembe,Lucas mwashamba watakunya povu maana itakuwa mwisho wa buku saba
 
Siyo tu kuona au kusimuliwa,
Ni mwanajeshi mpumbavu atawaza huo ujinga ,watu wanapombeka,wanadrive watoto wanasoma. Wanaishi makwao watake nini tena.

Serikali inawasikiliza.

Gwajima Shujaa wetu kachimba
Siku yako iwe njema mkuu
 
Wakuu, kwa hali ya kisiasa ya style hii katika nchi, kuna harufu pengine jeshi lililo upande wa wananchi likaingilia kati, ipo siku tutalala tukiongozwa na Rais tunayemjua tukaamka na mamlaka ya kijeshi kama ilivyo huko 🇧🇫, 🇲🇱 na 🇳🇪.
Mkuu naungana na wewe kwa asilimia mia nimewahi kuwaza hivi
Huko jeshini kuna binadamu pia na siyo wanyama
Kama vile huku mtaani jinsi tunavyosikitika na kuuumia kuhusu haya yanayoendelea basi kuna watu pia wenye mamlaka makubwa jeshini nao wanaumizwa sana na hii hali
 
Kwa mataifa madogo inawezekana,.
Kwa Tanzania ni ngumu.

Kwanza majeshi yenyewe ni matiiifu mno Kwa serikali yake
Mkuu ulitakiwa hilo neno 'matiifu mno' ulibold kisha ulifafanue, nipime kama ufafanuzi wako upo sahihi ama kama neno hilo unalielewa tofauti ili nami nichangiepo kidogo.
 
Ndugu yangu kwa hapa kwetu haita kaa itokee, niulize kwa nini?

Ni kwamba ukiangalia mfumo wa majeshi yetu ni kuwa wale wote wenye vyeo vikubwa huwa wanlipwa vizuri na wana marupu rupu ya kufa mtu , kuanzia magari mazuri nyumba za kuishi wakistaafu na fikiri hata wake zao inawezekana wanagawia mpaka taulo za kike

Sasa watu kama hao wataipigania tonge lao kwa kumwaga damu.
Ukiangalia hali ya sasa kama kweli tungekuwa na maafisa wa wanao jielewe kwenye taasisi zetu za ulinzi usingesikia haya yanayoendelea

Kila mtu mle kweye ngazi ya juu anaomba lau na yeye aonekane na mfalme lau aweze kuokota hata makombo toka kwa meza ya mfalme

Ni nani atasubutu kunyanyua mdomo wake huku tayari ana tonge mdomoni

Hawa wa chini ni akina kapuku tuu wakiambiwa muume mtu meno wao wanrukia kama mumbwa hana uwezo wa kuuliza kwa nini?
 
Izi nchi nyingi za Afrika utawala wa kijeshi nao sio, anaweza kuingia kwa nia njema ,ila akaamua kukengeuka pia.
Ila huwa najiuliza yale majaribu kwa mwl kwa wanaosema haiwezi kutokea, kwamba wale walikua wanatoka nje
 
Wakuu, kwa hali ya kisiasa ya style hii katika nchi, kuna harufu pengine jeshi lililo upande wa wananchi likaingilia kati, ipo siku tutalala tukiongozwa na Rais tunayemjua tukaamka na mamlaka ya kijeshi kama ilivyo huko 🇧🇫, 🇲🇱 na 🇳🇪.
Hiyo Serikali ya Kijeshi labda iongoze familia ya babaako na mamaako, lakini sio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Mark my words!!!
 
Nabashiri jambo baya au tusilolitazamia kutokea kwa sababu naona maamuzi mengi yanatolewa kwa gadhabu bila hata kufikiri kidogo repercussion. Jamani mimi sielewi tupo wapi na tunaelekea wapi kila kitu kipo shagalabagala. Hali hii naona Mungu ametuacha hakika.
 
Wakuu, kwa hali ya kisiasa ya style hii katika nchi, kuna harufu pengine jeshi lililo upande wa wananchi likaingilia kati, ipo siku tutalala tukiongozwa na Rais tunayemjua tukaamka na mamlaka ya kijeshi kama ilivyo huko 🇧🇫, 🇲🇱 na 🇳🇪.
Kuna tetesi waneongezewa mishahara
 
Sio rahisi kihivyo jeshi lenyewe ni toilet paper ya watawala si kirahisi hivyo
 
Back
Top Bottom