Mega project ya nini tena wakati miradi mikubwa bado inaendelea na haijakamilika, huu utaratibu ndio ulizuia ajira mpya,nyongeza za mishahara,kupanda madaraja na wastaafu kusotea pension zao maendeleo ya vitu bila maendeleo ya watu ni mateso makubwa sana.
Kuna Channel ya Tivii ilikuwa ina segment inaitwa kishindo cha awamu ya "gwala" yaani ni kila saa kinarudiwa si ni vyema maendeleo yakasemwa kwa watu.
Zaidi ya sgr,daraja la Busisi na Bwawa la Nyerere hakuna mradi mwingine mkubwa mkuu,miradi mingine ni ya kawaida tuu..
Pili mama keshaanza miradi mikubwa mipya na baadhi yake ni
1.Ujenzi wa Bwawa la Kidunda,zaidi ya Bil.400,
2.Ujenzi wa Bwawa la Farkwa.
3.Ujenzi wa airport na Ring Road Dodoma.,
4.Ujenzi wa miradi ya maji miji 28,zaidi ya Til.1
5.Mabarabara ndio kabisaa kila Kona ya Nchi ikiwemo DART awamu ya 3.
6.Ujenzi wa Hospital ya Kitaifa Mama na Mtoto Dodoma.
7.Ujenzi wa Hospital ya Kanda ya Magharibi Kigoma.
8.Ujenzi wa Chuo Maalumu cha Kitaifa cha TEHAMA Dodoma.
Kiufupi miradi ni countless across sectors.