Zikiwa zimebaki siku chache kufanyika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa, ni wananchi wachache sana ambao wamejitokeza kwenda kujiandikisha. Nilipojaribu kuwahamasisha wakajiandikishe, nilisikitishwa na nilichoambiwa.
1. Wananchi wengi miongoni mwa niliowauliza wanatambua umuhimu wa kupiga kura/kuchagua viongozi wao ili kuleta maendeleo.
2. Wananchi wengi wamekata tamaa kuona hata wakichagua kiongozi wanayemtaka, bado serikali/CCM ina viongozi wake na lazima wapite.
3. Wananchi wengi wanasema rushwa inafanya wapoteze haki yao.
4. Baadhi ya niliowauliza wanaogopa kuonyesha msimamo wao wa mgombea yupi/chama kipi wangekipigia kura kwa kuhofia usalama wao.
5. Wananchi wanaona viongozi wanaochaguliwa siyo waadilifu.
6. Wananchi wanaona viongozi wao wanatoa ahadi za uongo.
7. Wananchi wengi wameamua kupambania senti yao ya kila siku kuliko kupoteza muda kuchagua viongozi wasiokuwa na faida kwao.
8. Wananchi wengi maombi yao kwa Mungu ni afya na amani nchini.
Kipi kifanyike?
Viongozi badilikeni. Hata kama nafasi za kisiasa/uongozi ni biashara zenu na mmewekeza mitaji yenu, wananchi wengi wanatamani kuona ahadi zinatekelezeka.