Uchaguzi 2020 Kwa mwitikio uliopo kwenye mikutano ya upinzani, bado tunaamini wananchi wanahitaji kuhamasishwa na wasanii?

Uchaguzi 2020 Kwa mwitikio uliopo kwenye mikutano ya upinzani, bado tunaamini wananchi wanahitaji kuhamasishwa na wasanii?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Wakati CCM ikiangaika kukusanya wasanii kwenye mikutano vyama vingine vimeamua kujipima vinakubalika vipi bila kuwa na wasanii na bila kubeba wananchi kwenye malori.

Je. Kwa Hali hii mkakati wa ccm kubeba watu kwenye malori na kutumia wasanii unawasaidia kujua wanakubalika vipi au unawasaidia kujidanganya?

Je mpango mkakati wa miaka 5 ndo uliishia uwanja wa Uhuru? Kwenye mitandao hawapo, majukwaani hawapo wamepita kwa hisani ya tume, je lini wapiga kura watajisikia kushindanishwa?
 
Uchaguzi ni mikakati ndugu ! Hakuna cha kusingizia wasanii wala nini , wasanii ni sehemu ya jamii. Kama wapinzani wameshindwa kuwatumia ni wao! Wapinzani bado hawana mikakati madhibuti ya ushindi! Na imeonekana leo! Yan uzinduzi umekua wa hovyo tu!.
 
Kwetu vijana wa miaka ya 1990', wanasiasa wa Upinzani alikuwa Dr Wilbroad Peter Slaa na Mzalendo Zitto Ruyagwa Kabwe. Hao ndo watu waliokuwa wanakusanya Kijiji. Lowasa hakuwa mpinzan so hafai kuitwa mpinzan.
 
Natumai kesho jirani na uwanja wa jamuhuri kutakuwa na vituo vingi kushusha abiria, wenye mabasi Shabib na wengine wameombwa na kamati ya usafiri.
 
Natumai kesho jirani na uwanja wa jamuhuri kutakuwa na vituo vingi kushusha abiria, wenye mabasi Shabib na wengine wameombwa na kamati ya usafiri.
Nasikia uwanja wa barafu umekuwa "cleared" kwa ajili ya parking ya mabus na fuso za kuwabeba wanaokwenda Jamhuri.
 
Pale Mbagala niliona wasanii na mabasi pia ingawa watu hawakuwa wengi; nadhani hiyo ni sehemu ya mchakato wa kampeini zote za kisiasa. Halafu elewa mtandao sio unaoopiga kura; wingi wa wafuasi mtandaoni unaweza kudanganya kwani wafuasi wengine wako nje ya nchi, wengine ni watoto chini ya miaka 18.
 
CCM wanajua kabisa kuwa bila wasaniii,mikutano yao haiwezi kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi.
Kikubwa zaidi wanachotaka kuhalalisha kwa "nyomi ya kulazimisha", ni matokeo ya kupikwa ya "ushindi wa kishindo" wa ile idadi ya NEC ya nusu ya Watanzania kuwa 18+,na zaidi wote hao kuwa wamejiandikisha.
Justification.
 
Acha uongo
 
Ndiyo maana siwashabikii vitabu yenu alivyoandika muasisi wenu ni vizuri mno ila matendo yenu kwa raia wenzetu yanachefua yaani baada ya dhuluma ya kuwaengua au kutafuta mnathubu kujakutamba mitandaoni.
 
Uchaguzi ni mikakati ndugu ! Hakuna cha kusingizia wasanii wala nini , wasanii ni sehemu ya jamii. Kama wapinzani wameshindwa kuwatumia ni wao! Wapinzani bado hawana mikakati madhibuti ya ushindi! Na imeonekana leo! Yan uzinduzi umekua wa hovyo tu!.
Umeona eeeeh. Yaani wamechemsha sana hii siku ya ufunguzi.
 
Wananchi wana njaa, watahamasishwa na ubwabwa, tunamgonjea mzee wetu atangaze wapi tunalianzisha.
 
Ni kujitekenya na kucheke. Niwakumbushe watakaosombwa na malori kuandaa nauli ya kurudi makwao maana malori hayatawarudisha [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom