Kwa namna hii kweli viongozi wa Afrika watapata hata baraka kwa Mungu?

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Nimetembelea maeneo tofauti tofauti katika mwisho na mwanzo wa mwaka huu Tanzania na visiwani Zanzibar sio siri hali za uchumi wa mtu mmoja mmoja ni ngumu sana.


Watumisi ktk NGO's wanapunguzwa,
Wajasria mali wanalia hali ngumu ya biashara na utitiri wa kodi.
Wananchi wa chini kabisa mlo mmoja imekuwa kitendawili.


Najiuliza tu kama mtanzania mwenye haki ya kuzungumza kikatiba "JINSI HALI YA MAISHA ILIVYO NGUMU MITAANI ALAFU ETI UNASIKIA YAKUWA KODI HIZI HIZI ZA WANYONGE ZINATUMIKA KUWANUNUA VIONGOZI WETU KUTOKA VYAMA VILIVYOCHAFGULIWA NA WANANCHI WANYONGE NA MASKINI"?


Hivi kweli kwa hali hii hata viongozi, mataifa na bara la Africa kwa ujumla litapata baraka za Mungu kweli ?

Nimetumia tu haki yangu kikatiba kusema yanayonihusu sitaki povu kama nimekukwaza kaa kimya huenda ukawa hujatembea.
 
Viongozi wa afrika wengi wao hawapo kwa maslahi ya kuwaletea maendeleo wananchi. Bali kuiba na watu wa chama chake, ukiona kwenye siasa inatumika sisi CCM na wale Wapinzani. Ujuwe inatumika ile mbinu wagawe na uwatawale. Lakini ukisikia sisi sote Watanzania hapo ujuwe tumepata mleta maendeleo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…